Watendaji wa daftari la kudumu la mpiga kura wametakiwa kufanya kazi na Mawakala wa vyama vya siasa




Na Israel Mwaisaka,Nkadi

Watendaji wasaidizi wa daftari la kudumu la mpiga kura ngazi ya kata wilayani Nkasi wametakiwa kufanya kazi na Mawakala wa vyama vya siasa wakati wa uboreshaji wa taarifa kwenye daftari la kudumu la mpiga kura linalotarajia kuanza January 12 Hadi 18,2025.

Akizungumza na Watendaji hao wasaidizi wa daftari la kudumu la mpiga kura ngazi ya kata kufuatia mafunzo yanayoendelea mkurugenzi msaidizi idara ya daftari na Tehama Martin Mnyenyelwa amesema kuwa katika zoezi hili vyama vya siasa vimepewa jukumu la kupeleka Mawakala kwenye vituo vya uandikishaji kwa malengo mahususi ya kuhakikisha zoezi Hilo linafanyika kwa misingi iliyowekwa.


Amesema kuwa Mawakala katika zoezi Hilo kazi Yao kubwa ni kufuatilia uandikishaji ikiwa ni pamoja na kuwafahanu wakazi sahihi wa eneo husika Ili kukwepa kuwaandikisha Watu kwenye daftari la kudumu la wapiga kura ambao siyo raia wa Tanzania.

Sambamba na hayo pia amewataka Watendaji hao wasaidizi ngazi ya kata kuhakikisha wanavitunza vyema vifaa hivyo Ili viweze kuingia kwenye mzunguko wa Nne wa zoezi Hilo katika mikoa mingine kwani vifaa hivyo vya mafunzo vitazunguka Nchi nzima.



Hivyo amemtaka Kila mmoja kuzingatia kanuni ya Kila kitu anachokifanya katika uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura kwani Hilo ni zoezi muhimu Santa kwa taifa,hivyo hawataki kusikia kuwa mmoja wao ni kikwazo juu ya Hilo

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa