UTALII WA NYUKI HIFADHI ASILIA KALAMBO WASHIKA HATAMU
Wakala wa huduma za Misitu Tanzania (TFS) Wilayaya Kalambo Mkoani Rukwa Imeanzisha utalii wa Nyuki (AP TOURLISM) Ambao Utampatia fursaMtalii kujionea Shughuli za Ufugaji Nyuki Katika hifadhi ya Mazingira Asilia Kalambo ikiwa ni pamojana kudungishwa Nyuki Mwilini Ili Kuchochea na Kuimarisha Kinga za Mwili kwa watalii ambaowatakuwa wakitembelea hifadhi hiyo.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa utalii huo askari wa uhifadhi wa wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) Kalambo Daniel Dotto amesema katika kufanisha hilo serikali imeanzisha shamba maalum kwa ajili ya ufugaji nyuki na kutoa mizinga 500 yenye thamani ya shilingi million150 ambayo itawezesha watalii kujifunza namna bora ya ufugaji wa nyuki kisasa.
Amesema licha hilo mtalii ataweza kujionea mazingira halisi ya ufugaji nyuki na mazingira ikorojia ya msitu huo ikiwa ni pamoja na kutembelea maanguko ya maji ya mto Kalambo ambayo ni ya pili Afrika kwa urefu wa mita 235 kutoka maji yanapoanzia.
Kwa upande wake mhifadhi mkuu wa wakala wa hifadhi za misitu Tanzania TFS Ibrahim Mkiwa amesema licha ya hilo uwepo wa utalii huo utawezesha kuongezeka kwa mapato ya serikali Pamoja na watalii wanaotembelea hifadhi hiyo ambao kwa sasa wamefikia elfu moja (1000) kwa mwaka na kuwataka wananchi kuchangamkia fursa hiyo ili kujionea na kujifunza namna bora ya utengenezaji wa mizinga na ufugaji nyuki kisasa.Hata hivyo uanzishwaji wa utalii huo ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Mhe.Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuhamasisha wawekezaji na watalii kutembelea vivutio vya ndani.


Comments
Post a Comment