Radi yaua Ng'ombe 10 jamii yapata hofu



Na Israel Mwaisaka, Nkasi

NGO'MBE 10 wamekufa papo hapo baada ya kupigwa na radi Jana katika Kijiji cha Mwenge kata ya Kate wilayani Nkasi wakiwa marishoni.

Akizungumzia tukio hilo afisa Mtendaji wa kata ya Kate Deus William Njugu amesema kuwa Ng'ombe hao walipigwa na radi Jana majira ya saa 9 alasiri wakiwa marishoni na wakati radi hiyo inapiga palikua na Ng'ombe 15 na wote walindondoka chini lakini baada ya muda Ng'ombe 5 walisimama na kuondoka huku 10 wakipoteza maisha.

Amesema kuwa katika Ng'ombe hao waliokufa 5 ni madume na 5 ni majike na kuwa Ng'ombe hao wote ni Mali ya Steven Slanda mkazi wa Kijiji hicho cha Mwenge.



Afisa Mtendaji huyo wa kata amefafanua kuwa Ng'ombe hao wote Baada ya kufa kwa radi hiyo walianza kujaa matumbo,huku kijana aliyekua akiwachunga Ng'ombe hao akiwa salama.

Awali mwenyekiti wa Kijiji hicho cha Mwenge Charles Kafumu alikiri kutokea kwa tukio Hilo na kuwa matukio ya radi ya mara kwa mara ambayo yamekua yakitokea katika Kijiji hicho kusababisha madhara ikiwemo vifo imekuwa vikiwaweka njia Panda na hawajui Nini cha kufanya juu ya Hilo .

Amedai kuwa karibia Kila mwaka inapofika msimu wa mvua za masika ni lazima radi ipige na kusababisha madhara kwa jamii kama hayo ya kuuliwa kwa mifugo na hata binadamu au vyote kwa pamoja.

Afisa mifugo wa kata ya Kate Leticia Kahabi amesema kuwa kimsingi Ng'ombe hao hawatakiwi kuliwa kwani wana madhara ya kiafya na inabidi wafukiwe na asiwepo mtu mwenye uwezo wa kuweza kuipata nyama hiyo na kuitumia kama kitoweo.

Alidai kuwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za kiafya hairuhusiwi kula nyama ya mnyama ambaye hajachinjwa hivyo na kuwa mnyama akiuliwa na radi nyama yake Ina kuwa chembe chembe ya umeme wa radi ambao madhara yake uwa ni makubwa Sana kwa mtu anayekwenda kuitumia nyama hiyo kama kitoweo.

Diwani wa kata hiyo Dismas Msangawale amewataka wakazi wa Kate kuwa watulivu katika kipindi kama hiki linapotokea tukio la namna hiyo na kuacha kabisa kuhusisha matukio ya namna hiyo na Imani za kishirikina.

Na aliwataka Wananchi kuzingatia kanuni za kiafya kwa kufuata maelekezo ya Wataalamu juu ya kula nyama ya Ng'ombe hao waliopigwa na radi ikiwa ni pamoja na kutojaribu kufukua mizoga ya Ng'ombe hao kwa njia za kificho kwa lengo la kujipatia kitoweo kwani watakua wanajihatarisha wao kiafya.

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa