MAKINI TECHNOLOGY YAWASHIKA MKONO WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUMU



Na Israel Mwaisaka, Nkasi

TAASISI ya Watu makini Technology ya mjini Sumbawanga mkoani Rukwa kwa kushirikiana na Wadau wengine wametoa msaada kwa Wanafunzi 61 wenye mahitaji maalumu kama sehemu ya matendo ya huruma wanapouanza mwaka mpya wa 2025.

Akizungumza wakati wa kukabidhi misaada hiyo kwa Watoto hao katika shule tatu za mjini Namanyere wilayani Nkasi mkurugenzi wa Watu makini Technology Obeid Theofil Kasiano amesema kuwa taasisi yake kwa kushirikiana na timu ya vijana Wajasiliamali wamechangishana Tshs,1,386,000 na kuwanunulia mahitaji muhimu ya shule kama Madaftari,Rula,Kalamu na Pencils.

Amesema kuwa wao kama sehemu ya jamii wanaguswa na changamoto mbalimbali ambazo watu wengine wanakumbana nazo na ndiyo maana walionelea na wao kuweza kuwashika mkono Watoto wenye mahitaji maalumu kwa kuchangishana kidogo kile ambacho Mungu ameweza kuwaajalia kuweza kuvipata.



Shule zilizonufaika na msaada huo ni shule ya msingi Majengo,Isunta na Nkomolo ambapo Walimu wakuu wa shule hizo wamekua msaada mkubwa Katika kuwaainisha Watoto hao ambao wamekua wanufaika wa misaada hiyo.

Kasiano amefafanua kuwa kwao jambo Hilo imekuwa ni utaratibu wao ambapo kwa mwaka juu ni mara ya Sita na kwa wilaya Nkasi ni la Nne na kuwa wataendelea kufanya hivyo huku wakifanya ushawishi mkubwa kwa Watu wengine kuendelea kujitoa kama wao katika kuwasaidia Watu wenye uhitaji.


Amefafanua kuwa kitendo hicho cha kuwafanya Watu kujenga utamaduni wa kufanya matendo ya huruma unasaidia jamii kujengeka Katika upendo kitu ambacho kitapelekea jamii kuishi kwa Amani na kuchukuliana

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa