KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA TAMISEMI YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI MKOA WA RUKWA



Na Israel Mwaisaka,Rukwa

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imeridhishwa na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa Mkoani Rukwa. 

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo,  Jastin L. Nyamoga jana Januari 9, 2025 wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi ya sekta za afya, elimu, na miundombinu katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga, Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi, na Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga.


Akizungumza wakati wa ziara hiyo Nyamoga amesema Kamati imeshuhudia kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha nyingi katika sekta ya Afya, Elimu na Miundo Mbinu kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ambayo inalenga kutatua changamoto za wananchi wa Mkoa wa Rukwa. 


Amesema kamati imeridhishwa na ubora na  thamani ya fedha zilizotolewa katika miradi hiyo.

Naye, Naibu Waziri Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Mheshimiwa Zainab Katimba, ameipongeza Kamati ya Bunge kwa kazi nzuri ya ukaguzi wa miradi na kuihakikishia kamati kuwa Serikali itaendelea kupokea maoni, ushauri, na miongozo kutoka kwa Kamati ya Bunge na kuifanyia kazi ili kuboresha huduma kwa wananchi.

Ziara hiyo ilihusisha ukaguzi wa miradi  ya Hospitali ya Wilaya ya Nkasi,ufunguzi wa barabara ya Chala-Ifundwa,ujenzi wa shule mpya ya msingi Kituku, Wilaya ya Nkasi Hospitali ya Manispaa ya Sumbawanga,Barabara ya Malichewe kwa kiwango cha lami ,Shule ya Sekondari Itwelele,Kituo cha Afya Mpui Madaraja Matatu ya Upinde wa Mawe kwenye Barabara ya Laela-Kavifuti.


Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa