TANLAP- yawajengea uwezo Waandishi na Watangazaji kuhakikisha jamii inashiriki uchaguzi serikali za mitaa




Na Israel Mwaisaka,Dodoma

VYOMBO vya habari Nchini vinategemewa Kwa kiasi kikubwa katika kuuelimisha Umma na kutoa taarifa mbalimbali za uchaguzi wa serikali za mitaa ili kuhakikisha jamii inashiriki ipasavyo kwenye uchaguzi huo Ili kuweza kupata viongozi sahihi watakaowahudumia Wananchi katika ngazi ya serikali za mitaa.

Hayo yamesemwa na ofisa katika ofisi ya msemaji mkuu wa serikali Zamaradi Kawawa kwenye ufunguzi wa mafunzo Kwa Waandishi wa habari yaliyoandaliwa na shirika lisilokuwa la kiserikali TANLAP kwenye ukumbi wa African Dreams Jijini Dodoma yanayolenga kuwajengea uwezo Waandishi wa habari juu ya umuhimu wa Wananchi kushiriki kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa unatarajia kufanyika Desemba 27,2024.

Amesema kuwa vyombo vya habari kama vitatimiza wajibu wao vyema vitaisaidia jamii kuhakikisha kuwa inashiriki katika Kila hatua ya uchaguzi huo na kuwa jamii yenyewe ikiuelewa vyema mchakato na umuhimu wa uchaguzi huo Kila mtu atashiriki ipasavyo.

Kawawa alidai kuwa wao kama serikali wameona namna ambavyo vyombo vya habari vilivyotoa hamasa ya Watu kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la mkazi ambalo litawawezesha kushiriki kwenye uchaguzi na kuwa nguvu hiyo iliyotumika ikiendelea itawafanya Watu kujitokeza siku ya kupiga kura.





Awali mkurugenzi wa TANLAP Christina Ruhinda alidai kuwa mafunzo haya yametanguliwa na mafunzo Kwa Wasaidizi wa kisheria wapatao 225 na kuwa lengo la mafunzo hayo ni kutaka kuona namna ambavyo Watu walijitokeza kujiandikisha ndivyo wajitokeze kupiga kura Kwa wingi.

Alidai kuwa Waandishi wa habari Kwa kushirikiana na Taasisi zisizokuwa za kiserikali zilizopewa vibali vya kutoa elimu wakijenga umoja itasaidia Kwa kiasi kikubwa jamii kupata uelewa mkubwa juu ya umuhimu wa ushiriki kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa baada ya kupata uelewa wa kutosha.


Amefafanua kuwa mradi Huu umelenga kuwasaidia Watu wa makundi mbalimbali ya Wanawake,Vijana na Walemavu katika kuona kwamba Kila mmoja anashiriki ipasavyo kwenye uchaguzi huo wa Serikali za mitaa.

Katika mafunzo hayo Waandishi wa habari na Watangazaji walikumbushwa kanuni mbalimbali za uandishi na utangazaji na kubwa ni kuhakikisha kuwa Kila kinacholipotiwa kinachochea amani na utulivu.


Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa