RAIS DKT. SAMIA JINSI ALIVYOPAMBANIA MIUNDOMBINU YA BARABARA KUONGEZA TIJA YA KIUCHUMI NCHINI.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais.Dkt. Samia Suluhu,imefanikiwa kujenga barabara za lami za umbali wa Kilometa 819.22 na kuongeza za kiwango cha changarawe,hali iliyoongeza fulsa za kiuchumi.
Ujenzi wa barabara na mijini na vijijini zimefungua fursa za kiuchumi kwa kwa wananchi wa kada mbalimbali wakiwemo wakulima ambao wamekua wakisafirisha mazao yao kwenda kuuza kwenye masoko ya ndani na nje.
Kabla Rais Dkt,Samia hajaingia madarakani hali ya barabara hasa katika maeneo ya vijijini zilikuwa na changamoto,lakini tangu mama Samia aingie madarani kilometa nyingi zimejengwa kwa Lami,Chang alawe na vumbi.
Maeneo mengi ambapo barabara zimejengwa kwa changalawe au vumbi zimekuwa zikipitika vizuri huku serikali ikiwa katika harakati za kutafuta fedha kujenga barabara za Lami.
Ujenzi wa barabara hizo umeongeza ambapo mtandao wa barabara za lami ni kutoka kilometa 2,404.90 hadi kufikia kilometa 3,224.12.hi vi sasa.
Ujenzi wa barabara za changarawe kilometa 11,924.36 na hivyo kuongezeka kwa mtandao wa barabara za changarawe kutoka kilometa 29,183.17 hadi kilometa 41,107.52.katika kipindi hiki.
Mbali na ujenzi wa barabara hizo,pia wakala wa Barabara (TARURA) wameweza kujenga madaraja makubwa sita (6) ambayo ni ya Berega (140m) (Kilosa,) Msadya (60m) (Mpimbwe DC), Mwasanga (40m) (Mbeya) ambayo tayari yameanza kutumika.
Aidha ujenzi wa madaraja ya Kiwila (40m)-Ileje,mkoani Songwe, Mkomanzi-Korogwe mkoani Tanga (60m) na Kalambo mkoani Rukwa (80m)-(Kalambo), unaendelea.
Uongozi waTARURA umeeleza kuwa, katika kupunguza gharama, wameazimia kujenga barabara na madaraja kwa kutumia malighafi zinazopatikana maeneo ya kazi kama mawe, matofali ya kuchoma.
Kwa ujenzi wa barabara kwa kutumia mawe,mpaka sasa jumla ya kilometa 23.18 za barabara za mawe zimejengwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 8.1 ambapo ni sawa na Shilingi. Bilioni 12.8 kama wangetumia lami nyepesi (double surface dressing) na Shilingi. Bilioni 33.6 kama wangetumia lami ya zege (Asphat Concrete).
Ujenzi wa madaraja kwa kutumia mawe mojawapo ya kipaumbele cha TARURA ni kutumia malighafi zinazopatikana maeneo ya kazi ili kupata ufanisi wa gharama za ujenzi.
Hadi mwezi Februari, 2024 TARURA ilijenga madaraja 226 ya mawe yenye thamani ya Shilingi Bilioni 12.52 ambapo gharama imepungua kwa zaidi ya asilimia 50.
Ujenzi wa barabara kwa kutumia teknologia mbadala, Wakala unaendelea kufanya majaribio ya teknolojia mbalimbali ili kutumia udongo uliopo eneo la kazi badala ya kusomba kutoka maeneo mengine ya mbali.
Hadi sasa kwa kutumia Teknolojia ya ECOROADS zimejengwa Km 22 na ujenzi upo katika hatua mbalimbali za ukamilishaji.V.
Matengenezo ya Barabara - kilometa 21,500 zimefanyiwa matenge nezo na kilometa 21,057.08 zipo katika hatua mbalimbali za ukami lishaji.VI. na kwamba hayo ni machache katika makubwa yaliyo fanyika.





Comments
Post a Comment