Polisi waomba taarifa za vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia ili kutokomeza vitendo hivyo



Na Ibrahim Yassin, Songwe.

Imeelezwa kuwa ulinzi wa nchi ni wetu sote hivyo jeshi la polisi limeitaka jamii kutoa taarifa za vitendo vyote vya ukatili wa kijinsia na Unyanyasaji dhidi ya Watoto pamoja na kutoa taarifa za Wahalifu na Uhalifu ambao unatokea kwenye himaya zetu ili kuweza kuzishughulikia kwa haraka.

Hayo amezungumzwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Augustino Senga jana Novemba 08, 2024 katika Msikiti wa Tahadia uliyopo mjini Tunduma mkoani Songwe.



Vilevile Kamanda Senga alitoa rai kwa waumini hao kuacha tabia zisizofaa ambayo zinaweza kusababisha migogoro na vifo katika jamii, Pia aliwaomba viongozi wa msikiti huo kukemea vitendo hivyo.

Pia amewataka waumini hao kushiriki kwa amani katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakofanyika tarene 27 mwezi wa 11 mwaka huu na kuw achagua viongozi waadilifu kwa mstakabali wa maendeleo ya maeneo yao.


Sambamba na hayo Kamanda Senga alipongezwa kwa elimu aliyoitoa msikitini hapo na Sheikh Mkuu wa Mkoa Wa Songwe Husein Issa Batuza na alichukua fursa hiyo kumuomba Kamanda Senga kuendelea kuhubiri na kukemea uovu ili jamii ibadirike na kuachana na maovu.

Sheikh Batuza aliwataka waumini hao kuendelea kueneza amani na upendo kama dini yao inavyowataka ikiwa ni pamoja na kushiriki katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika hali ya amani na kuchagua viongozi ambao watakuwa na tija katika maeneo yao.



Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa