HALMASHAURI YA WILAYA NKASI YAWEKA MIKAKATI MADHUBUTI YA MAKUSANYO YA NDANI




Na Israel Mwaisaka,Nkasi

MKURUGENZI mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Nkasi Afraha Hassan amesema kuwa Halmashauri yake imejipanga ipasavyo katika eneo la ukusanyaji wa mapato na kuwa Hadi Sasa katika robo ya kwanza ya mwaka 2024/25 wamevuka lengo la ukusanyaji Kwa kufikia 32%.

Amesema kuwa amekaa na Watendaji wote wa kata na kuwekeana mikakati ya kuhakikisha mapato yanakusanywa na kuwa hatakua na huruma Kwa mtu yeyote atakayezembea katika eneo Hilo na kuwa katika kufanikisha Hilo ofisi yake itahakikisha madai yao yote yanalipwa Kwa wakati na zoezi Hilo limekwisha Anza.

Hayo ameyasema kwenye kikao Cha Baraza la Madiwani Cha kujadili taarifa za robo ya kwanza Kwa mwaka wa fedha wa 2024/25 ni baada ya kupokea taarifa za kwenye kata ambapo Madiwani katika taarifa zao walijikita kutoa taarifa za makusanyo katika kata zao katika kipindi Cha miezi mitatu iliyopita.

Hilo lilikuja baada ya Madiwani kusisitiza suala la makusanyo ya ndani na kumtaka mkurugenzi mtendaji awe mkali Kwa Watendaji wake katika suala Zima la makusanyo na kuomba iwepo motisha Kwa Watendaji wanaokusanya vizuri mapato.

Diwani wa kata ya Chala Michael Mwanalinze alidai kuwa mipango yote ya maendeleo katika wilaya Ili itekelezeke inahitaji fedha ambapo aliwaomba Madiwani wenzie kuwa sambamba na Watendaji wao katika suala Zima la ukusanyaji wa mapato.


Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Pankrasi Maliyatabu Kwa upande wake amemtaka Kila mmoja kuwajibika ipasavyo katika nafasi yake huku Watendaji wa kata wakipewa jukumu Hilo la kuhakikisha mapato hayapotei.

Pia aliwataka Watendaji hao wa kata kuwasimamia viongozi wa vijiji katika maeneo yao kuona wanawasomea Wananchi wao mapato na matumizi Ili kuondoa manung'uniko Kwa Wananchi Kwa kutosomewa mapato na matumizi katika vijiji vyao





Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa