DC ITUDA AKUTANA NA VIONGOZI WAPYA WA WACHIMBA MADINI WATETA JAMBO.



Na Ibrahim Yassin, Songwe. 

Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Mhe. Solomon Itunda amefanya kikao na viongozi wapya wa  wachimbaji Wadogo wa Madini  Mkoa wa Songwe (SOREMA)  kujadili mikakati endelevu namna ya kuwawezesha wachimbaji wadogo wa madini ya Dhahabu kuongeza uzalishaji.

Viongozi hao waliochaguliwa walifanya kikao na mkuu wa wilaya wakiwa na ajenda nyingi za maboresho katika sekta yao ikiwemo upatikanaji wa kiwanja kwa ajili ya kujenga ofisi ya kudumu.

Mhe. Itunda alikutana na viongozi hao jana katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Songwe iliyopo Mkwajuni ambapo alipongeza uongozi huo kwa kuweza kuchaguliwa baadhi ya wajumbe kuingia katika kamati za FEMATA.




Mkuu huyo wa Wilaya amewaahidi viongozi hao kuwa maombi yao yatafanyiwa kazi kwa haraka ikiwa ni pamoja na kupata uwanja wa kujenga ofisi za SOREMA.

Pia, Mhe. Itunda amemshukuru Rais wa JMT, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha sekta ya madini ikiwa ni pamoja na uimarishaji wa mifumo na masoko hali inayosaidia kuleta tija kwa wachimbaji na kupunguza utoroshwaji wa madini.



''Masoko haya tuyatumie vizuri kuongeza pato la Taifa,halmashauri na wachimbaji wenyewe hali inayorahisisha pia kupata takwimu sahihi za madini, hali hii pia imepunguza utoroshwaji madini na wachimbaji kuuza madini yao kwa usalama zaidi kwa bei elekezi''amesem Dc Itunda..

 Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Songwe ndugu Chone Malembo amempongeza mkuu wa wilaya hiyo kwa kuona umuhimu wa chama hicho cha wachimbaji na kwamba endapo watapatiwa uwanja na kujenga ofisi itarahisisha ufanyaji kazi wao.

Katika kikao hicho, Mhe.Dc-pamoja na Afisa madini Malembo walijadili mambo mbalimbali ambayo yanalenga kuwasaidia wachimbaji wa madini Wilaya ya Songwe kuongeza uzalishaji kwa wachimbaji na kuongeza pato la serikali kupitia toza na ushuru wa madini.





















Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa