Wakulima Songwe baada ya kunufaika na zao la ufuta sasa wageukia kilimo cha Mbaazi
Na Ibrahim Yassin,Songwe
WANANCHI jamii ya wakulima wilayani Songwe mkoani hapa kuanza kunufaika na kilimo cha zao la mbaazi baada ya kupata Bilioni 31 kwenye zao la ufuta kupitia mfumo wa stakabadhi gharani huku halmashauri ikipata Bil,1 za ushuru.
Asilimia 75 ya wananchi wa Songwe wanaendesha masiaha yao ya kila siku kwa kutegemea kilimo,ufugaji,uchimbaji madini na uvuvi,hivyo mpango wa serikali kupitia halmashauri hiyo kuwawezesha mbegu na pembejeo kumeongeza chachu ya kilimo chenye tija.
Ili kuendana na kasi ya serikali ya Rais Dkt,Samia ya kuwapaisha kimaisha wananchi kupitia kilimo,hatimaye halmashauri ya Songwe ilienda kujifunza kilimo bora cha mbaazi huku ikijipanga kuongeza bajeti kwenye ununuzi wa mbegu na kuwagawia wakulima.
Afisa kilimo wilayani Songwe Iddy Ramadhani alisema sababu kubwa ya wakulima kupata fedha nyingi ni kutokana na Rais Dkt,Samia kuwawezesha mafunzo na vitendea kazi zikiwemo pikipiki maafisa kilimo ambao wameweza kuwatembelea wakulima na kuwapa ushauri.
Alisema mfumo wa stakabadhi ghalani umewawezesha wakulima kuuza mazao likiwemo zao la Ufuta kwa bei nzuri huku usalama wa fedha zao ukiimalika kwa kuwa wanaingiziwa kwenye akaunti zao za benki.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo,Secilia Kavishe akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana alisema licha ya wilaya hiyo kuwa ni ya kimadini walianzisha mfumo wa stakabadhi ghalani na kuwawezesha wakulima kuwapa mbegu bure na hivi sasa baada ya kujifunza kilimo cha mbaazi wanatarajia kuwapa mashamba na mbegu ili waanze kulima.

Comments
Post a Comment