Shule yapongezwa kwa kuanzisha miradi ili kujikwamua kiuchumi

 



Na Ibrahim Yassin, Mbozi.

IMEELEZWA kuwa kuanzishwa kwa miradi mbalimbali katika shule ya sekondari Ndugu iliyopo wilayani Mbozi mkoani Songwe ni moja ya chanzo muhimu cha kujiongezea kipato shuleni hapo.

Akizungumza jana Octoba 9/2024 wakati wa mahafari ya 15 ya kuwaaga wanafunzi wa kidato cha nne, makamu mkuu wa shule hiyo Mwl, Janeth Mwamwite amesema lengo la kuanzisha miradi hiyo ni kuongeza kipato cha shule.

Amesema shule hiyo ilijengwa kwa nguvu za wananchi huku serikali ikikamilisha na kupeleka wafanyakazi (Walimu) ambapo ilipata usajili wa namba S2789 mwezi Machi 15/2007.

Amesema miaka inavyozidi kwenda idadi ya ufauru inazidi kuongezeka ukilinganisha na ilivyokuwa mwaka 2019 na kwamba mitihani ya Taifa kipindi cha miaka 3 mfululizo imeshika nafasi za tatu katika shule za serikali.

Amesema katika kipindi cha miaka 3 mfululizo wamepata asilimia 90 ya ufauru sababu kubwa ni kuweka kambi kwa ajili ya kujisomea madarasa ya mitihani yaani kidato cha 4 na cha 2.

( Leo tarehe 9 tunafanya sherehe za kuwaaga wanafunzi 209 kati ya hao wamaume ni 66 ambapo idadi yao imepungua kutokana na uhamisho na utoro" )amesema.

Ameongeza kuwa katika kuhakikisha wanafunzi wanapata lishe bora wakati wote  wameanzisha miradi itakayopelekea wanafunzi waongeze usikivu darasani kwa kupata mlo kamili.



Aliitaja miradi hiyo kuwa ni shamba la Kahawa linalosimamiwa na City Cofee ya jijini Mbeya ambao wamekuwa wakishiriki kwa ukaribu maendeleo na taaluma ya shule.

Pia aliongeza kuwa wameongeza kuboresha mazingira ya shule kwa kupanda miti ya kivuli,matunda, mbao na kilimo cha mboga mboga pamoja na kufungua duka la shule.

Sambamba na hilo pia amesema wamefanikiwa kuchimba kisima kirefu cha maji kilichopunguza gharama za uendeshaji kutokana na bili za maji.

Alitaja changamoto zilizopo kuwa ni ukosefu wa thamani za walimu kama viti, meza,kabati na vyumba vingi vya madarasa vikiwa chakavu hivyo vinatakiwa vikarabatiwe.

Alizungumza kwenye mahafari hayo, Diwani wa kata ya Nyimbili ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji wa makampuni ya Lima Limited aliyekuwa mgeni rasmi katika mahafari hayo ameahidi kuunga mkono utatuzi wa changamoto hizo.



Nzunda amesema yeye kitaaluma.ni mwalimu hivyo anatarajia kuona wanafunzi wanapata alam A na B na alama C ziwe.chache na kwamba alama D hataki kuziona huku akiwatakia heri katika mitihani yao.

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa