Polisi Rukwa wazindua kampeni ya "Tuwaambie kabla hawajaharibiwa" ili kuleta chachu ya mabadiliko katika jamii na kupambana na vitendo vya ukatili
Na Israel Mwaisaka,Rukwa
JESHI la Polisi mkoani Rukwa Jana limezindua kampeni ya "Tuwaambie kabla hawajaharibiwa " yenye lengo la kuwalinda vijana dhidi ya changamoto mbalimbali zinazoweza kuathiri fikra na tabia zao.
Uzinduzi huo uliofanyika wilayani Nkasi na mkuu wa wilaya Peter Lijualikali kuwa mgeni rasmi ulienda sambamba na kutoka elimu katika mada mbalimbali ikiwemo ya ukatili wa kijinsia,Dawati la jinsia na Watoto maana na kazi zake,Uzalendo na tunu ya taifa,ukatili wa kijinsia Kwa njia ya mtandao ikiwa ni pamoja na rushwa ya ngono..
Akitoa taarifa juu ya mpango huo kamanda wa Polisi mkoani Rukwa ( SACP) Shadrack Masija alisema kuwa mpango huo umelenga kuwa msingi wa kuzuia vitendo vya ukatili na unyanyasaji katika jamii ya Tanzania .
Alisema kuwa kampeni hii imelenga zaidi kuwasaidia Wanafunzi waliopo shule za Sekondari,vyuo vya kati na vyuo vikuu ili kuwa na uwezo wa kukabiliana na changamoto zinazowakumba pale wanapoanza masomo yao na ukichukulia kwamba katika umri huo ukutana na mabadiliko mbalimbali ya kimwili na kuwa kampeni hiyo itasaidia kuweza kupunguza mihemko ya vijana na kuwa salama .
Alidai kuwa kampeni hiyo Kwa kiasi kikubwa inalenga kuwa msingi wa kuzuia vitendo vya ukatili na unyanyasaji ikiwa ni pamoja na kuwajenga kiakili na kitabia Ili waweze kuepuka athari mbaya za mazungira wanayokutana nayo.
Akizindua rasmi kampeni hiyo mkuu wa wilaya Nkasi Peter Lijualikali alisisitiza umuhimu wa kushirikiana na Jeshi la Polisi kupitia kamisheni ya Polisi jamii na Dawati la jinsia na Watoto huku akiwataka Wanafunzi na Wazazi kuunga mkono jitihada hizi Ili kuweza kuyafikia malengo yaliyowekwa katika kampeni hiyo ya kuhakikisha vijana wote wanakua salama.
Alisema kuwa serikali imekuwa katika jitihada mbalimbali za kuwalinda vijana na Watoto Kwa kutunga Sheria Kali na mambo mengine mengi na kuwa kampeni hii ya Polisi ya " Waambie kabla hawajaharibiwa" inakwenda kuongeza Chachu ya mapambano hayo na kutaka Kila mmoja serikali katika nafasi yake kuunga mkono jitihada hizo Ili kuweza kukabiliana na vitendo vya ukatili katika jamii yetu.
Awali mkuu wa Dawati la jinsia na Watoto mrakibu msaidizi wa Polisi (ACP) Faustina Mwakapangala alisema kuwa kampeni hiyo "Tuwaambie kabla Hawajaharibiwa"inatarajia kuwa na Chachu ya mabadiliko katika jamii Kwa kuwajenga Wanafunzi na vijana ujasiri wa kukabiliana na changamoto zinazowakabili huku ililenga kuleta matokeo chanya Kwa vizazi vijavyo.
Alidai kuwa kampeni hii kitaifa ilizunduliwa mkoani Njombe Agosti 29,2024 na wao wanaungana na Jeshi Hilo kitaifa kwa uzinduzi wa kampeni hii mkoani Rukwa ni Moja ya mikakati ya kuwalinda vijana na kuepuka vitendo vya ukatili vinavyowazunguka kulingana na umri wao wenye mihemuko mingi
Aidha mkuu wa Dawati la jinsia na Watoto wilaya Nkasi Mkaguzi msaidizi wa Polisi Atupele Mwakaliku pamoja na afisa wa Polisi jamii mkoa Rukwa kamishina msaidizi wa Polisi Zacharia Bura walidai kuwa mahudhurio makubwa ya Watu kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo ni ishara ya mapokeo mazuri na kuwa jamii itatoa ushirikiano wa kutosha na kuwepo Kwa uhakika wa kukabiliana na vitendo vya ukatili na kuwepo Kwa maadili mema Kwa vijana .
Walisema kuwa vita hiyo ni kubwa lakini itakua nyepesi kama Kila mmoja katika nafasi yake atawajibika ipasavyo hasa Kwa kuondoa ukimya Kwa vijana na kuwaanbia ukweli vitu wasivyostahili kuvifanya katika umri wao Bali wasubiri wakati na Kwa kufanya hivyo kutawafanya vijana kuwa salama na kuzifikia ndoto walizonazo katika maisha yao.





Comments
Post a Comment