MJUMBE TAASISI YA MWL-NYERERE APONGEZA SHULE KUFUNGA MASHINE NA BWAWA LA SAMAKI

MKUU WA SHULE AOMBA MIL, 3 UNUNUZI WA MOTA ASEMA MIRADI HIYO ITAONGEZA CHA CHU KWA WANAFUNZI.


Na Ibrahim Yassin, Songwe

MJUMBE wa taasisi ya Mwl,.Nyerere na Diwani kata ya Nyimbili wilayani Mbozi mkoani Songwe Mwl,Tinson Nzunda amewapongeza walimu wa shule ya sekondari Ndugu kwa kubuni vyanzo vya mapato vitakavyopaisha uchumi wa shule hiyo.

Mwl, Nzunda ameyasema hayo jana Octoba 9/2024 wakati wa sherehe za mahafari ya 15 ya kuwaaga wanafunzi wa kidato cha 4 katika shule hiyo.

Awali akizungumza Katika mahafari hayo, kaimu mkuu wa shule hiyo Mwl,.Janeth Mwamwite amesema  waliamua kubuni miradi katika shule hiyo ili kuongeza tija ya uelewa kwa wanafunzi.



Alisema siku za hivi karibuni walinunua mashine za kukoboa na kusaga ili waweze kusaga nafaka lwa ajili ya chakula cha wanafunzi pamoja na kusaga nafaka za watu wengine ili kujiingizia kipato.

Amesema hivi sasa  wanahitaji Tsh, 300.000 kwa ajili ya ununuzi wa Mota ili wazifunge mashine hizo na kwamba pia wameweza kununua Ng'ombe wa maziwa wa Tsh, Milioni 1.9 ili wanafunzi wapate chai asubuhi.



Mbali na hilo pia amesema wamechimba bwawa la kufugia samaki na tayari wamefuga samaki wanaendelea kukua hii yote ni kuhakikisha wana funzi wanapata mlo kamili na kuongeza uelewa darasani.

Hata hivyo mkuu huyo wa shule amesema katika kutambua umuhimu wa afya wamepanda miti ya matunda ya aina mbalimbali ili wanafunzi wajimw ambafai na pia shamba la kahawa likiwa linaend rlea kustawi.

Baada ya maelezo hayo, Mgeni rasmi Nzunda amepongeza hatua hiyo na kuahidi kuungana na shule hiyo ili kufanikisha malengo yao,.huku akiwataka wananchi kuunga mkono jitihada hizo.


"Mimi ni mgeni rasmi mmesema mnahitaji kukam iliaha ujenzi wa bweni, ninayoa tofari 10.000 zeny e thamani ya Milioni1 kukamilisha ujenzi huo huk u akiahidi kuendelea kusaidia zaidi ili shule hiyo itimize malengo yao.


Hata hivyo ujenzi wa miradi hiyo itasaidia kuweze sha kupaa kwa ufauru wa shule hiyo na pia shule zingine zinatakiwa kuiga mfumo wa shule hiyo.

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa