Diwani Nzunda aipiga jeki shule ya sekondari Ndugu kwa kutoa tofali 10,000 na apongeza shule kujikwamua kiuchumi



Na Ibrahim Yassin, Mbozi

DIWANI wa kata ya Nyimbili wilayani Mbozi mkoani Songwe Mwl, Tinson Nzunda ametoa tofali 10.000 zenye thamani ya Tsh, Milioni 1.kusaidia ujenzi wa hosteli katika.shule ya sekondari Ndugu.

Mwl, Nzunda ametoa msaada huo baada ya kupokea Risala ya shule hiyo jana October 9/2024 kwenye mahafari ya 15 ya kuwaaga wanafunzi wa kidato cha 4 shuleni hapo.

Mwl.Nzunda, ambaye pia ni mjumbe wa taasisi ya Mwl, Nyerere na mkurugenzi wa kampuni za Lima Limited amesema kitaaluma yeye ni mwalimu hivyo amewataka wanafunzi kutumia taaluma waliyonayo kuishi vizuri na jamii huko waendako.

Mwl, Nzunda ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya elimu katika halmashauri ya wilaya ya Mbozi amesema yupo tayari kuchangia shughuri za maendeleo pale atakapo hitajika


Amesema atafurahi endapo wanafunzi wote watachaguliwa kujiunga na kidato cha tano, pia aliwapongeza jinsi walivyoweza kutengeneza sabuni na bidhaa zingine akiwataka wakautumie ujuzi huo pindi wawapo nyumbani.

Kaimu mkuu wa shule hiyo Mwl, Janeth Mwamwita amesema anauhakika wanafunzi watafanya vizuri mitihani yao na kwamba anapongeza mgeni rasmi kwa kutoa tofari hizo zitakazosaidia kumalizia jengo la hostel.

Akisoma risala ya shule hiyo Lestyuta Kandonga ambaye ni mwanafunzi kidato cha 4 amesema pamoja na changamoto zilizopo wanahitaji tofari kumalizia ujenzi wa bweni ili wanafunzi wa kike waweze kulala shuleni hapo.

Pia alimueleza mgeni rasmi kuwa kitaaluma wapo vizuri pia wamekuwa wakishiriki michezo ya Umiseta na kufanya vizuri hivyo amesema hawatamuangusha katika mitihani wanayotarajia kuifanya siku za hivi karibuni.


Akizungumza kwa niaba ya wazazi waliofika kwenye mahafari hayo Anne Mwampashi amesema amefarijika na muenendo mzuri wa shule hiyo huku akimpongeza diwani Nzunda kwa misaada ya shuleni hapo.



Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa