BAADA YA KUNUFAIKA NA ZAO LA UFUTA SONGWE SASA KUANZA NA KILIMO CHA MBAAZI.




Na Ibrahim Yassin,Songwe

WANANCHI jamii ya wakulima wilayani Songwe mkoani hapa kuanza kunufaika na kilimo cha zao la mbaazi baada ya kupata Bilioni 31 kwenye zao la ufuta kupitia mfumo wa stakabadhi gharani huku halmashauri ikipata Bil,1 za ushuru.

Asilimia 75 ya wananchi wa Songwe wanaendesha maisha yao ya kila siku kwa kutegemea kilimo,ufugaji,uchimbaji madini na uvuvi,hivyo mpango wa serikali kupitia halmashauri hiyo kuwawezesha mbegu na pembejeo kumeongeza chachu ya kilimo chenye tija.

Ili kuendana na kasi ya serikali ya Rais Dkt,Samia ya kuwapaisha kimasha wananchi kupitia kilimo,hatimaye halmashauri ya Songwe ilienda kujifunza kilimo bora cha mbaazi huku ikijipanga kuongeza bajeti kwenye ununuzi wa mbegu na kuwagawia wakulima.

Afisa kilimo wilayani Songwe Iddy Ramadhani alisema sababu kubwa ya wakulima kupata fedha nyingi ni kutokana na Rais Dkt,Samia kuwawezesha mafunzo na vitendea kazi zikiwemo pikipiki maafisa kilimo ambao wameweza kuwatembelea wakulima na kuwapa ushauri.

Alisema mfumo wa stakabadhi ghalani umewawezesha wakulima kuuza mazao likiwemo zao la Ufuta kwa bei nzuri huku usalama wa fedha zao ukiimalika kwa kuwa wanaingiziwa kwenye akaunti zao za benki.



Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo,Secilia Kavishe,alisema licha ya wilaya hiyo kuwa ni ya kimadini walianzisha mfumo wa stakabadhi ghalani na kuwawezesha wakulima kuwapa mbegu bure na hivi sasa baada ya kujifunza kilimo cha mom wanatarajia kuwapa mashamba na mbegu ili waanze kulima.

Aliongeza kuwa mwaka 2022/2023 walizalisha kilo 7,556,510 za ufuta ambapo mikopo ilitolewa zaidi ya Tsh,200,000,000 kutoka benki,katika mauzo hayo,halmashauri ilipata ushuru Tsh,792,291,513 huku wakipata Tsh, Bilioni.28.

Alisema msimu wa mwaka 2023/2024 uzalishaji ulikuwa kilo 8,361,797 mikopo yenye thamani ya Tsh,Bilioni 3.4 ilitolewa na benki,katika mauzo ya ufuta halmashauri ilikusanya ushuru Tsh,969,334,065,vyama vya ushirika (AMCOS) vilipata Tsh,585,334,065 na fedha ya wakulima ilikuwa Tsh,31,365,137,633.

Amesema katika msimu huu kuna mazao mengine likiwemo zao la mbaazi litaingizwa kwenye mfumo wa stakabadhi ghalani kwani walienda wilaya ya Babati na Hanang kujifunza,kwa sasa wapo kutoa elimu na watagawa mbegu na mashamba watu walime.



Mkuu wa wilaya hiyo,Solomon Itunda alisema wilaya ya Songwe kwa sasa imetulia vijana wamejikita kwenye uzalishaji mali ikiwemo kilimo huku halmashauri ikiwawezesha mbegu bora na kwamba mkakati uliopo ni kuhamasisha wakulima wengi kujiunga kwenye vyama vya ushirika.

Alisema kupitia mfumo wa stakabadhi gharani halmashauri ilipata ushuru wa Bilioni 1 wakulima Bilioni 31 na kuwa  hicho ni chanzo muhimu kinachotakiwa kutilia mkazo huku akifurahia ushirikiano mzuri uliopo baina yake na viongozi wengine.


Akizungumza kwaniaba ya wakulima wengine,Anastazia Kalinga mkazi wa kijiji cha Patamela alisema yeye ni mmoja wa wanufaika wa zao hilo na pia ameweza kupelekwa kujifunza kilimo bora na halma shauri mkoani Morogoro hivyo ombi lao kuu ni kuwahishiwa mbegu na pembejeo mapema.


Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa