BARABARA YA CHANG'OMBE -MAGAMBA KUJENGWA KUONGEZA FURSA ZA KIUCHUMI.



Na Ibrahim Yassin,Songwe 

IMEELEZWA kuwa kukamilika kwa barabara ya Magamba -Chang'ombe kutaongeza fursa za kiuchumi hasa kwa kusafirisha mazao kwenda mikoani.

Asilimia 75 ya wakazi wilayani Songwe wanaendesha maisha yao  kwa kutegemea kilimo ufugaji na uchimbaji madini ya dhahabu hivyo barabara hiyo imetajwa kuwa na umuhimu  mkubwa.

Hayo yamezungumzwa jana na mkuu wa wilaya ya Songwe Solomon Itunda wakati mwenge wa uhuru ukikagua mradi huo.





Itunda alisema  barabara hiyo ni muhimu hasa kwa usafirishaji wa nafaka, abiria na kuunganisha wananchi wa kata jirani ambao wanategemeana  katika mahitaji muhimu ikiwemo shule huku akimuomba mkimbiza mwenge aikague njia hiyo.

Naye meneja wa wakala wa barsbara vijijini na mijini ( TARURA) wilayani humo, Mhandisi Emmanuel Nkwera, alisema barabara hiyo muhimu ilikatika mwaka 2022 baada ya mvua  za mafuriko kunyesha.

Alisema kukatika kwa barabara hiyo mwaka 2024 fedha zilipatikana na mwezi Mei 2024 mkandarasi alipatikana na mkataba ukasainiwa kwa ajili ya kuanza kazi hiyo ya ujenzi.

Alisema ujenzi umeanza kwa kujengwa box karavati ujenzi unaotekelezwa kwa fedha za ufadhili kutoka Benki ya Dunia kupitia mradi wa "Rise" na ulianza mwezi Mei 31/2024.




Mhandisi Nkwera alimueleza mkimbiza mwenge kitaifa kuwa mradi huo unatekelezwa na kampuni ya CHAGATU EARTHWORKS ya jijini Mbeya kwa Tshs, 446,012,662,00 .

Alisema kwa mujibu wa mkataba mdomo mmoja wa kalavati na ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilometa 1 kiwango cha changalawe.

Aliongeza kuwa hatua iliyojengwa kwa sasa ni kusafisha eneo la ujenzi,kuchimba msingi wa boksi kalavati ,kupanga mawe na kumimina zege kwa ajili ya blinding na usukaji nondo na kumimina zege kwa ajili ya kuta.

Mbunge wa jimbo la Songwe Philipo Mulugo alisema kwa namna ya kipekee anawapongeza Tarura kwa hatua waliyofikia hivyo anaamini barabara ikikamilika itarejesha mawasiliano yaliyo katika




Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa. Eliakim Mzava licha ya kuikagua barabara hiyo alitoa rai kwa viongozi wilayani Songwe kuhakikisha wan atumia mfumo wa Nest kufanya manunuzi na kuweka wazi matangazo ya utoaji tenda ili kupata kampuni na mkandarasi mwenye uwezo na vigezo.

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa