Wanakijiji wajitolea kujenga jengo la kujifungulia kina Mama kuhepuka vifo pingamizi vya uzazi kufuata huduma kilometa 8



Na Ibrahim Yassin.Songwe.

WANANCHI 1235 wa vitongoji 4 vya kijiji cha Mpapa kata ya Mpapa bonde la Kamsamba wilayani Momba mkoani Songwe wamechangishana fedha kujenga jengo la mama na mtoto kuhepuka vifo wakitembea kilometa 8 hadi kituo cha afya Kam samba.

Asilimia 80 ya wakazi vitongoji hivyo 4 vya Namaimba,Chinyuwanda,Nambizo na Mpapa kati wanaendesha maisha yao wakitegemea kilimo na ufugaji huku wakikabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa huduma hiyo.

Ukosefu wa huduma hiyo ya jengo la mama na mtoto kulipelekea akina mama kutembea umbali huo hadi Kamsamba kufuata huduma ya kujifun gua huku wengi wao wakijifungulia njiani hasa nyakati za usiku.

Hayo wameyasema leo August 17/2024 katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na mdau wa maendeleo na mkulima bora wa bonde la Kamsam ba uliolenga kuwaunganisha wakulima uliofanyika makao makuu ya kata ya Mpapa.

Lengo la kuwaunganisha wakulima ni kutaka kuwa na umoja wao ili kuhepuka kudalaliwa na viongozi wa kisiasa wanaowahujumu kwa kivuli cha stakabadhi gahalani huku shehena za ufuta zikisafirishwa bandarini wakulima wakiwa hoi kiuchumi.

Fumbo Sichalwe mkazi wa Mpapa amesema kero hiyo imewaumiza muda mrefu na kupokea mapen dekezo na ushauri wa kujenga jengo hilo toka kwa Abdul Ntilo mkulima bora.

Willehelledy Kashampamba mwenyekiti wa CHADEMA kata ya Mpapa amesema alipopata taarifa juu ya kuchangia hakusita kwani aliona jinsi akina mama wanavyopata shida na kwamba kukamilika kwa mradi huo wataondokana na kadhia hiyo.




Akizungumzia mikakati ya jengo hilo afisa mtendaji wa kijiji cha Mpapa Joseph Nsalamba amesema akina mama wameteseka vya kutosha na sasa watapata huduma za mama na mtoto kwenye zahanati hiyo kwani ujenzi utakamilika muda mfupi.

Amesema katika zahanati hiyo chumba cha kujifungulia kipo kimoja hivyo kinazidiwa na jengo jipya litakuwa na vyumba 3 chumba cha kujifungulia, kupumzikia mjamzito, stoo na sehemu ya kukaa muuguzi.

Amesema hadi sasa kiasi cha Tsh. Milioni 3 zitokanazo na michango ya wananchi zimetumika na ujenzi upo hatua ya renta huku wakiomba wadau wawape sapoti kwa ajili ya umaliziaji.

Mkulima bora wa bonde hilo la Kamsamba Abdul Ntilo alipotembelea jengo hilo alisifu maamuzi ya wananchi huku akitoa Tsh,200.000 kusaidia ujenzi na kuahidi kutafuta wadau watakaosaidia kupiga ripu.

Ntilo ambaye mwaka 2020 aligombea udiwani wa kata hiyo ya Mpapa kupitia Chadema amesema maendeleo hayana vyama hivyo aliwataka wadau pasipo kujali vyama waungane kutatua changamoto za kina mama na za wilaya kwa ujumla.

" Maendeleo hayana chama ,mimi ni Chadema lialia lakini linapokuja suala la maendeleo tuweke vyama pembeni tuchape kazi, nafahamu jinsi wak ukima walivyotumika kama daraja la wanasiasa tukiunda umoja hilo litakwisha" amesema.


Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa