VIONGOZI TUMIENI UBUNIFU KUONGEZA UFANISI KAZINI – CP HAMAD.




Na Ibrahim Yassin.Songwe 

Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Hamad Khamis amewataka viongozi wa Jeshi la Polisi kutumia maono na vipaji walivyonavyo kubuni mambo mbalimbali katika Vitengo wanavyoviongoza ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya kazi za kila siku.

Hamad ametoa rai hiyo leo Agosti 17/2924 katika Chuo cha Polisi Zanzibar wakati alipokuwa akizun gumza na Maofisa, Wakaguzi na Askari wa Jeshi la Polisi katika hafla ya kumuaga aliyekuwa Mkuu wa Chuo hicho Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polidi SACP Augostino Senga.



Senga ambaye hivi karibuni alihamishiwa Mkoa wa Songwe kuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo.

Kamishna Hamad alisifu juhudi na ubunifu wa SACP SENGA katika kuimarisha miundombinu ya barabara zenye kiwango cha lami pamoja na ujenzi na ukarabati wa majengo katika chuo cha Polisi Zanzibar.

Nae SACP SENGA amewashukuru Maafisa, Wakaguzi na Askari wa Chuo cha Polisi na Kamisheni ya Polisi Zanzibar kwa kumpa ushirikiano wakati akiwa Mkuu wa Chuo hicho.





Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa