Serikali yakifungia kiwanda cha kutengeneza pombe kali kwa kutofuata kanuni za uanzishwaji wake



Na Baraka Lusajo,Rukwa

Serikali imekifungia kiwanda cha kutengeneza pombe kali aina ya banana kilichopo katika kata ya Ulumi wilayani Kalambo mkoani Rukwa kisha kumkamata mmiliki wa kiwanda hicho Nichoraus Shirima kutokana na kuanzisha kiwanda bila kuwa na vibali sambasamba na kutengeza pombe zinazodaiwa kuwa hatari kwa afya za watumiaji.

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Kalambo Shafii Mpenda akiwa ofisini kwake amesema wamekifungia Kiwanda hicho kutokana na kutokuwa na vigezo ikiwemo mazingira duni ya uzalishaji bidhaa,mazingira machafu,pamoja na ukosefu wa nyaraka muhimu za uanzishaji wa kiwanda kutoka kwenye mamlaka husika.

Licha ya hilo amesema baada ya kufanya ufuatiliaji wa kina kwa kushirikina na vyombo vya usalama walibaini mwekezaji huyo kusambaza na kuzalisha bidhaa kinyume cha sheria na kusema halmashauri haina mgogoro na wawekezaji na badala yake inasisistiza wawekezaji kufuata sheria na taratibu za uwekezaji.

‘’kwa kushirikina na vyombo vya usalama baada ya kufika pale tulibaini uzalishaji wa kreti 300 za pombe na baada ya upekuzi wa kina tulibaini mwekezaji huyo anafanya biashara hiyo pasipo kufuata taratibu kwani hata Halmashauri tulikuwa hatuna taarifa zake kwani hata ukiangalia kiwanda chake kilikuwa na uzalishaji mkubwa licha ya kuwa na muonekano mdogo’’ Alisema Mpenda.

Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha usafi na mazingira wilayani humo Richard Manuma amesema wawekezaji hawana budi kufuata sheria za usafi wa mazingira wakati wa uanzishaji viwanda ili kuepuka milipuko ya magonjwa

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa