RC SONGWE AIPONGEZA HALMSHAURI YA KALAMBO KWA UBUNIFU TEKNOLOJIA YA UKAUSHAJI SAMAKI NA DAGAA



Na Baraka Lusajo,Mbeya

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Daniel  Chongoro ameipongeza Halmashauri ya Kalambo mkoani Rukwa kwa kuanzisha teknolojia mpya ya ukaushaji wa dagaa na samaki  kwa kutumia kaushio la kisasa (solar tent drier) ambalo litawezesha upatikanaji  wa samaki  na dagaa wenye ubora na kuwezesha wavuvi kujikwamua na hali ya kiuchumi.

Ameyasema hayo baada ya kutembelea banda la Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo kupitia maonesho ya wakulima nanenane yanayofanyika kikanda Jijini Mbeya na kuipongeza Halmashauri ya Wilaya Kalambo kwa kuanzisha teknolojia hiyo ambayo itaweszeha kupunguza upotevu wa mazao ya uvuvi baada ya kuvuliwa hususani kipindi cha masika.


Awali akitoa taarifa kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Shafi Mpenda ,Afisa uvuvi wilayani humo  Bw. Abdul Balozi ,Amesema sambamba na teknolojia hiyo pia wameleta bidhaa mpya ya unga wa samaki  ambayo ni ya kwanza kwa kanda ya nyanda za juu kusini ambayo itasaidia kupunguza udumavu na utapia mlo kwa watoto kutokana na unga huo kuwa na virutubisho vyote.

‘’Unga huu utaweza kutumiwa na watu wote ikiwemo watoto wachanga,na watu wazima na katika kuhakikisha huduma hii inapatika sehemu zote za mwambao wa ziwa Tanganyika kwa kushirikina na mradi wa FISH4ACP tumejenga makaushio makubwa matatu na jiko moja la kubanikia samaki katika vijiji vya Kasanga, Kilewani na Samazi’’,alisema  Bw. Balozi.  

Kwa upande wake mkuu wa Divisheni ya kilimo , mifugo na uvuvi Bw. Nicholas Mrango amesema licha ya hilo Halmshauri imetenga fedha milion sitini na moja ( 61,000,000/=) kwa ajili ya  utekelezaji wa afua za lishe ikiwemo kutoa elimu kwa jamii juu ya matumizi sahihi ya vyakula bora kwa lengo la kutokomeza tatizo la udumavu wilayani humo.

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa