POLISI SONGWE WAPIGWA MSASA KUELEKEA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA



Na Ibrahim Yassin.Songwe

Mkuu wa kitengo cha kampuni binafsi za ulinzi na Polisi Wasaidizi kutoka makao makuu ya Jeshi la Polisi Dodoma, kamisheni ya Polisi jamii Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Ulrich Matei akiwa na viongozi wengine kutoka makao makuu ya polisi Dodoma wametoa elimu na mafunzo kwa askari mkoani Songwe.


Kamishna Matei akiambatana na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Paul Sanga kutoka Kamisheni ya Operesheni na Mafunzo Agosti 21, 2024 wamefanya ziara ya kikazi Mkoani Songwe na kutoa elimu kuhusu mambo mbalimbali yakiwemo maandalizi ya uchaguzi.




DCP Matei aliwaelekeza askari kutambua wajibu wao katika uchaguzi na kutojihusisha na itikadi za kisiasa bali kutenda haki bila ya kujali itikadi za Vyama vya kisiasa, Dini, Jinsia au Kabila.

Kikoa hicho kilifanyika ukumbi wa Polisi Vwawa Wilaya ya Mbozi na kuudhuriwa na Jeshi la Mage reza, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Idara ya uhamiaji na Jeshi la Akiba (Mgambo).




Katika semina hiyo jeshi la polisi pia walishiriki mazoezi mbalimbali yakiwemo ya ukakamavu huku wakionesha utayari wa kufanya kazi kwa weredi.



Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa