Ntila awapigia magoti Wananchi akiwapa pole kufanyiwa udalali zao la ufuta
Na Ibrahim Yassin.Songwe
Mwanakijiji mzalendo na mkulima bora wa Bonde la Kamsamba anayetoka kijiji cha Mkonko kata ya Mpapa wilayani Momba mkoani Songwe, Abdul Ntila amewapa pole wananchi kutokana na kufanyiwa udalali wa zao la ufuta.
Zao la ufuta ni zao muhimu na la kiuchumi wilayani humo ambalo liliingizwa kwenye mfumo wa stakabadhi Gharani toka msimu uliopita lakini kumeibuka sintofahamu nyingi juu ya mfumo huo.
Ntila ameyasema hayo leo August 6/2024 alipokuwa kwenye mikutano ya hadhara kwenye vijiji vya kata hiyo akihamasisha wakulima kuunda umoja wao huku akiwataja viongozi wa kisiasa wilayani humo kujihusisha na udalali kuwanyonya wakulima.
Amesema mfumo wa stakabadhi gharani haujawa sawa kwa wilaya ya Momba kwani umewekwa bila wakulima kupewa elimu juu ya umuhimu wa kuuza mazao yao kwa mfumo huo huku wakiendelea kutaabika.
Ameongeza kwa kuwataka wakulima kuanzisha umoja wao na kuchagua viongozi akiwemo mwenyekiti wa wakulima kama ilivyo kwa wafanyabiashara, wavuvi, Umoja wa madereva na wengineo huku yeye akijitolea kuwa makamu mwenyekiti.
Amesema lengo la kuanzisha umoja huo kutarah sisha wakulima kupanga mambo yao kabla ya kuamua ama kuamrishwa kufanya jambo fulani hali itakayozuia unyonyaji uliopo.
"Ndugu wananchi leo nimewaita waandishi wa habari ili taarifa hizi zimfikie Rais wetu kipenzi Dkt, Samia Suluhu ili ajue jinsi wakulima wa zao la Ufuta wanavyonyonywa na viongozi wa kisiasa wakihusika"amesema.
Amesema lengo kuu ni kutaka mkulima auze mazao yake anapotaka aangalie ni bei ipi itamfaa kuliko kulazimishwa kuuza pahala fulani na kwamba wakati wa kuandaa mashamba mkulima asumbuliwi.
Amesema mkulima anapoandaa shamba, analima anapanda mbegu ,anakopa hela za kumsaidia kazi zake zifanikiwe hakuna stakabadhi ghalani wala mwanasiasa au kiongozi yeyote anayejitokeza kumsaidia,akianza kuvuna wajinatokeza na kumpangia sehemu ya kuuza.
"Ndugu wakulima katika bonde lote hili la Kamsamba ufuta unalazimishwa ukauzwe stakabadhi garani tena kwa bei ndogo haizidi 40.000 kwa debe na hela uipati kwa wakati, kule Kilyamatundu kuna kampuni inanunua ufuta hadi 60.000 hii ni haki ? amesema.
Akizungumza kwaniaba ya wakulima wenzake kwenye mkutano huo, Samwel Mtafya amesema wanahitaji elimu zaidi kuhusu mfumo huo na ili mkulima asiendelee kunyonywa ni lazima waungane na kuunda uongozi utakaowasimamia mambo yao

Comments
Post a Comment