Nkasi wafanya tathimini ya dira ya maendeleo ya taifa ya mwaka 2050



Na Israel Mwaisaka,Nkasi

WAJUMBE wa kamati ya ushauri ya wilaya Nkasi wakiongozwa na mwenyekiti wa kikao Levocatus Chikala aliyemwakilisha mkuu wa wilaya Peter Lijualikali wamefanya tathimini ya maendeleo ya dira ya taifa kwa kuangazia nyanja za kiuchumi,Kisiasa,Utawala bora pamoja na amani na utulivu.

Kupitia kikao hicho Wajumbe wameipongeza serikali kwa utekelezaji mzuri wa dira ya maendeleo ya taifa ya mwaka 2025, ambapo serikali imeleta maendeleo makubwa kwa kujenga na kuboresha miundo mbinu ya barabara ,Maji,Umeme,Madarasa pamoja na hospitali.

Vile vile imehakikisha amani na utulivu kwa kushirikisha vyama vya siasa katika kujadili maendeleo pamoja na kudumisha ushirikiano kati ya sekta binafsi na taasisi za serikali.

Pamoja na hayo Wajumbe wametoa mapendekezo ya Dira ya taifa ya maendeleo kwa mwaka 2050 iendelee kujikita katika vipaumbele stahiki ikiwa ni pamoja na kuboresha sekta ya usafiri wa anga,sekta ya


kilimo,kuweka mpango kazi wenye vipaumbele kulingana na mazingira unalinda maadili kulingana na mila na desturi za watu wa Nkasi na mkoa Rukwa kwa ujumla.

Kwa upande wake kaimu mkurugenzi mtendaji wa wilaya Steward Vidoga amewashukuru wajumbe kwa kuchangia maoni ya mapendekezo Ya dira ya taifa ya maendeleo ya mwaka 2050 na kuwaasa kuendelea kulinda maadili,Amani na utulivu kwa kuzingatia usawa bila kujali itikadi za kidini ,siasa wala kabila.

Aidha Vidoga amehimiza ushirikiano kwa serikali katika hatua mbalimbali zinazoendelea katika kujenga taifa ikiwa ni pamoja na maboresho kupitia miradi ya maendeleo na wataalamu katika sekta zote

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa