NFRA Yawatahadharisha Vishoka ununuzi wa mahindi wao wapanga kununua tani 137,000
Na Ibrahim Yassin,Songwe
WAKATI wakala wa chakula nchini (NFRA) ikiendelea kununua mahindi ya wakulima mkoani Songwe madalali au vishoka wanaowadalalia wakulima wamepewa angalizo la kutombughudhi mkulima.
Serikali kupitia wakala wa chakula nchini imepanga kununua tani 137. 000 za mahindi ya wakulima ambapo kilo 1 inanunuliwa kwa Tsh, 700 na hadi jana tani 28.000 zimekwisha nunuliwa.
Hata hivyo katika zoezi hilo kulikuwepo na viashiria vya madalali kujipenyeza kuwalaghai wakulima lakini hilo limedhibitiwa na wakulima wanaouza mazao yao kwa amani.
Akizungumza leo Agosti 29/8/2024 meneja wa kanda wa wakala wa chakula nchini Jofrey Lupenza amesema zoezi la ununuzi linaendelea vyema na wanatarajia kununua tani 137.000 za mahindi huku tani 28.000 zikiwa tayari zimenunuliwa.
Alisema mahindi waliyonunua awali nchi ya Zambia wameiuzia Tani 55.000 na wanatarajia kuyabeba siku yeyote kuanzia leo na kwamba muitikio wa wakulima kuwauzia mahindi upo vizuri ukilinganisha na ilivyokuwa awali.
Aliongeza kuwa wanapokea gunia chini ya 1000 wale wenye gunia nyingi wanapewa mifuko kisha wanafuatwa majumbani ili kuepuka foleni na kwa siku wananunua tani 1000 hadi 12000 kwa kanda nzima.
Alisema kulikuwa na sintofahamu hapo nyuma baada ya baadhi ya wakulima kupeleka mahindi machafu hivyo wakawapa maelekezo kuwa wayachambue na ikiwezekana yaliyo shambani mabunzi ya mahindi yaliyooza wasichanganye na mazuri.
"Tunanunua mahindi yaliyo mazuri tunapima kwenye mizani Digitali ,mizani ya kawaida inatumika pindi ya Dijitali inapoharibika,mkulima hatozwi fedha ila kama mahindi machafu anayasafisha kutumia vibarua anawalipa "alisema.
Aliongeza kuwa kituo cha Kakozi mahindi yananunuliwa na muwekezaji raia wa nchini India kwa kilo Tsh 550 wao NFRA wananunua kwa Tsh, 700 na wanalipa ndani ya siku 14 hivyo wakulima wanatakiwa kupeleka mahindi yaliyo safi.
Ezekiel Mwampashi mkulima alisema ameuza gunia elfu 2 na amelipwa ndani ya siku 14 na kwamba utaratibu uliopo ni mzuri huku akiipongeza seri kali kwa kuongeza bei kutoka Tsh, 600 hadi Tsh,70 0 kwa kilo.



Comments
Post a Comment