NANYARO AWAASA VIJANA KUTOKAA VIJIWENI KUPIGA SOGA AWATAKA WAJIUNGE KWENYE VIKUNDI VYA UZALISHAJI MALI.
Na Ibrahim Yassin,Songwe
VIJANA nchini wametakiwa kutokaa vijiweni kupiga soga za umbea na badala yake wajiunge au waanzishe vikundi vya uzalishaji mali na kukop esheka vitakavyo waondoa kwenye lindi la umasikini.
Kauli hiyo imetolewa leo Agosti 28/2024 na mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM mkoani Songwe Alipozungumza nao katika kata za Msangano Tindingoma na Mkulwe wilayani Momba mkoani Songwe.
Alisema imekuwa ni kawaida vijana kupenda kukaa vijiweni badala ya kujiingiza kwenye utafutaji fedha kupitia kilimo,Uvuvi, Ufugaji Viwanda na biashara na kwamba uenda wanafanya hivyo kutokana na kukosa watu wa kuwashika mkono.
Nanyaro ambaye pia ni mdau wa maendeleo wa nyanda za juu kusini aliwataka vijana hao kuunda vikundi na kujisajiri ili waweze kupata mikopo ya halmashauri na hata ya kwenye taasisi za kifedha na kuanzisha miradi.
"Undeni vikundi mvisajili anzisheni miradi mimi kama kiongozi nitawapambania mpate mikopo na kizuri zaidi Rais Dkt Samia Suluhu amerudisha ile mikopo ya asilimia 10, changamkeni msipitwe na fursa hiyo"alisema Nanyaro.
Juma Mwashilindi mkazi Msangano alisema ushauri wa mjumbe huyo unamashiko hivyo watajitahidi kuhamasishana kuunda vikundi na kuvisajili pale watakapopata changamoto ya mitaji wataomba msaada.
Julia's Kandonga mkazi wa Mkulwe alisema watahakikisha wanaunda vikundi ili wapate mitaji kupitia taasisi za kifedha na kwamba watahitaji kupatiwa elimu ya uelewa juu ya kuanzisha miradi.
Nae Hilda Simfukwe mkazi wa Naming'ong:'o alis ema ni wazo zuri ila upatikanaji wa mitaji ni tatizo endapo wataunda vikundi na kuvisajili watamuona mjumbe huyo ili awape muongozo.
"Binafsi namfahamu Mdau huyu wa maendeleo ni mtu wa kujitolea kwani alikarabati bweni la wanafunzi, aliweka mfumo wa maji safi ya bomba ,aliwanunulia Compute na Printa wanafunzi shule ya Kamsamba" alisema Simfukwe.
Simfukwe,mbali na hilo alisema Mdau Nanyaro ni mtu na nusu kwani aliweza kutoa tofali na fedha kuanzisha ujenzi nyumba ya mtumishi wa CCM Sumbawanga Rukwa , amewasaidia vijana wa boda boda mkoani Katavi kusajili vikundi na Mama lishe Iringa kwa kuwapatia mitaji.




Comments
Post a Comment