NANYARO AHAMASISHA UPANDAJI MITI WAZEE WA MILA WAKIADHIMISHA SIKU YAO YA UPENDO.
Na Ibrahim Yassin.Songwe
MJUMBE wa halmashauri kuu CCM mkoa wa Songwe Ombeni Nanyaro amemuomba mkuu wa wilaya ya Momba Elias Mwandobo kuuenzi mwenge wa uhuru kwa kuhamasisha kila kaya kupanda miti na kutunza mazingira.
Nanyaro ameyasema hayo jana katika sherehe zilizowakutanisha pamoja kati ya viongozi wa chama na serikali na viongozi wa mila kujadili mambo mbalimbali ikiwemo mmomonyoko wa maadili kwa jamii.
Maadhimisho ya siku ya wazee wa mila yalifanyika wilayani Momba mkoani humo ambapo viongozi wa chama na serikali walionekana kuunga mkono jitihada za wazee hao kusaidia ulinzi wa nchi kwa kukemea mabaya.
Alisema ipo haja ya kuuenzi mwenge wa uhuru kwa kuhamasisha upandaji wa miti kuepuka uharibifu wa mazingira,kujihadhari na mabadiriko ya tabia nchi ikiwemo kudhibiti ukataji miti ovyo.
"Mkuu wa wilaya hamasa ifanyike kwa kila kaya ipande japo mti mmoja kwani itasaidia kudhibiti mabadiliko ya tabia nchi na hata wanaoharubu mazingira kwa kukata miti wadhibitiwe.
Nae chifu Malinga Mkoma wa 7 wa wilayani humo alisema wazo la mjumbe Nanyoro linapaswa kufa nyiwa kazi kwani miti ni uhai na wanaoharibu mazingira wanatakiwa wadhibitiwe.
"Leo tunaadhimisha siku yetu ya upendo, tutakuombea Taifa hili na wanyama wote waliopo ili waishi maisha marefu, tutaendelea kuenzi mila na tamaduni zetu na kukataza mabaya"alisema Chifu Malinga.
Alisema baadhi ya watu sio waaminifu wamekuwa wakikata miti na kuchoma mkaa wakizidi kuharibu mazingira hivyo kasi ya katazo iongezeke na hamasa ya upandaji miti iongezwe kulinda mazingira na uoto wa asili.
Mkuu wa wilaya hiyo Elias Mwandobo ameyapokea mawazo hayo na kusema wazee wa mila wanapaswa kuheshimiwa ndiyo maana hata Rais Dkt Samia aliwaita Ikulu kuzungumza nao ambapo walimbatiza jina la Chifu Hangaya.
Alisema mjumbe wa halmashauri ya mkoa Mr, Omneni amejitolea kusaidia wanafunzi shule ya kamsamba inatakiwa iungwe mkono kwa kupele ka wanafunzi kusoma.
"Wazee wa mila tusaidieni mmomonyoko wa maadili umeshika kasi tuwalee na kuwalinda watoto dhidi ya ukatili, na kufuatilia nyendo zao yakiwemo masomo , vitendo vya ubakaji na ulawiti havitakiwi"alisema Dc Mwandobo.
Alisema kuna sehemu alikuta watu wamekata miti alipowauliza alisema eti wanawinda Panya na kwamba msako wa nyumba kwa nyumba utaanza kusaka wanaoharibu mazingira.
Aliongeza kuwa wale watoto wanatakiwa kusoma na kulindwa ili wawe viongozi wa baadae tuepuke mila potofu zikiwemo za ndoa za jinsia moja tuzienzi mila na tamaduni za kitanzania.



Comments
Post a Comment