Mwili wa mtu aliyeuawa na kutumbukizwa kwenye kisima waopolewa


MWILI wa mtu aliyeuawa ajulikanaye kwa jina la Daniel Siyame mkazi wa Ilembo Vwawa umeopolewa leo kwenye kisima katika kitongoji cha Ilolo shuleni kata ya Ilolo wilaya ya Mbozi mkoani Songwe...anaripoti Ibrahim Yassin.

Mwenyekiti wa kitongoji cha Ilolo Shuleni Yutas Mkondya amesema amepokea taarifa za tukio hilo majira ya Saa moja asubuhi kuwa Kuna mwili upo kwenye kisima Cha mtu mmoja ambaye ni Fundi umeme.

Mkondya amesema baada ya kufika eneo la tukio na kutoa taarifa Kwa Jeshi la Zimamoto na uokoaji na Jeshi la Polisi ambapo wote walifika Kwa wakati na kuuchukua mwili huo na kuupeleka hospitali ya Wilaya ya Mbozi.

Aidha ametowa wito kwa wananchi kuendelea kufunika visima vyao ili kuepusha majanga kama hayo kwani kumekuwa na matukio mengi ya watu kufa kwenye maji.

Akizungumza kwa niaba ya Jeshi la Zimamoto na uokoaji Mkoani Songwe. Sajent Ahobhokile Lugembe kutoka Jeshi la Zimamoto na uokoaji mkoani Songwe amesema wataendelea kutoa elimu kila inapohitajika Ili kudhibiti majanga hayo.

Mwili huo umeopolewa ikiwa ni siku chache kupita baada ya mwili wa mwanamke Clara Nzunda mkazi wa kata hiyo kuopolewa Julai 30,2024 kwenye Bwawa lililopo Tacri Mbimba.

Hata hivyo katika siku za hivi karibuni wilayani Mbozi kulipotiwa mauaji ya kikatili ya watu kujichukulia sheria mkononi ambapo watu wawili katika matukio yanayofanana waliuawa na wananchi wenye hasira.

Watu hao ambao majina yao hayakufahamika mmoja aliuawa kisha mwili wake kuchomwa moto na kutupwa katika kitongoji cha Mpakani karibu na reli ya Tazara kata ya Hasanga akituhumiwa kujaribu kuiba.

Diwani wa kata ya Hasanga Maliki Nzoa alipopata taarifa hizo alifika eneo la tukio akiwa na polisi kata huku akidai mwili huo ulichukuliwa kwa uchunguzi wa jeshi la polisi.

Tulio lingine lilitokea katika kijiji cha Igale kata ya Iyula baada ya watu wenye hasira kali kumuua mwanaume ambaye jina lake halikufahamika kwa tuhuma za kujaribu kuiba katika soko la Ngeze.

Diwani wa kata hiyo  ya Iyula Charles Shonza alisema mtu huyo alishambuliwa usiku akidaiwa kuiba baada ya mlinzi wa soko hilo kupiga mayowe akiomba msaada.

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa