Mjane apewa haki na mahakama kuu na kukabidhiwa ardhi aliyokuwa ameporwa
Na Ibrahim Yassin.Songwe
MAHAKAMA kuu kanda wa Mbeya jana ilimpa ushindi Mariam Kalipande (Mjane) katika kesi ya rufaa namba 64/ya mwaka 2023 iliyohusu mgo goro wa ardhi.
Kesi hiyo ilihusisha mgogoro wa ardhi kati ya Rozina Kalupande ambaye ni kaka wa marehemu Retson Kalupande aliyedaiwa kubadilisha hati ya familia baada ya kaka yake kufariki dunia na kuandika jina la Taasisi kinyume na taratibu.
Baada ya Rozana kufanya hivyo mjane Mariam alifungua kesi katika baraza la ardhi na ilipotoka hukumu baraza la ardhi la wilaya ya Mbozi lilimpa ushindi mama huyo Mariam.
Katika kesi hiyo mama Mariam alimshitaki wifi yake Rozama ambaye ndiye anayeiendesha Taasisi ya Wakina iliyoasisiwa na kaka yake,pamoja na Serikali ya kijiji cha Haraka ikiwemo halmashauri ya wilaya ya Mbozi kwa kosa la kubadilisha umiliki.
Baada ya ushindi huo walalamikiwa hawakuridhika na hukumu hivyo walikata Rufaa mahakama kuu kanda ya Mbeya wakipinga baraza la ardhi kumpa ushindi Mjane huyo.
Kesi upande wa walalamikaji ilisimamiwa na mawakili Jery January akiwa upande wa halmashauri ya Mbozi na Omari Ndamungu akiwa upande wa Taasiisi ya Wakina Mama na watoto Foundation huku wakili Baraka Mbwilo akimsimamia Mjane Mariamu.
Kesi hiyo ilianza kusikilizwa Mwezi September 5 /2023 na kutolewa hukumu Julai/9/2024 huku Mariam Kalupande na mumewe ambaye ni matr ehem Letson Kalupande kupewa ushindi.
Wakili upande wa mrufani aliiambia mahakama hiyo kuwa baraza la ardhi halikuwa na uwezo wa kusikiliza shauri hilo namba 4 ya mwaka 2017 kwa kuwa mwanasheria wa serikali hakuunganishwa kama sehemu ya walalamikiwa.
Nae wakili mwingine upande wa warufani alikazia akisema katika kesi zinazohusu mali za serikali ilitakiwa mwanasheria mkuu wa serikali ajulis hwe na awe ni sehemu ya walalamikiwa.
Akitafsiri sheria hiyo wakili Baraka Mbwilo anayemsimamia mrufani wa (Mjane) akiunga mkono uwepo wa sheria hiyo huku akisema wakati inaanza kufanya kazi tayari kesi ilikuwa imefunguliwa.
Alisema wakati sheria hiyo inapitishwa iliandikwa na kutangazwa kwenye gazeti la serikali February 21/2020 wakati tayari kesi iliisha funguliwa mwaka 2017.
Baada ya tafsiri hizo za kisheria Jaji wa mahakama hiyo V.M Nongwa alisema ni kweli sheria hiyo ipo na kwa kuwa kesi ilifunguliwa kabla ya sheria hiyo kuanza kufanya kazi mahakama inaitupilia mbali kesi hiyo hivyo mrufaniwa ndiye mwenye uhalali wa kumiliki ardhi hiyo.
Alisema marehemu Letson Kalupande alilipata eneo hilo kutoka kwa Shangali Halinga ambapo alianzisha Taasisi hiyo ya Wakina ikiwa tayari ene o hilo palijengwa mashine 2 za kusaga na eneo hilo hilo ndipo zilikuwepo ofisi za Taassi hiyo.

Comments
Post a Comment