Mbunge Mwandabila akerwa na kituo cha afya kutokuwa na umeme ampigia simu meneja Tanesco kujua umeme utawekwa lini?



Na Ibrahim Yassn Songwe.

Mbunge viti maalum mkoani Songwe Neema Mwandabila leo August 6/2024 ametembelea kituo cha afya Mwaka kati kilichopo halmashauri ya mji Tunduma na kubaini ukosefu wa umeme.

Kituo hicho cha afya ni muarobaini muhimu kwa wakazi wa kata hiyo ya Mwaka kati ambao walikuwa wakitembea umbali mrefu hadi kituo cha afya Tunduma kusaka tiba kwa kutembea umbali wa kilometa 3.

Kituo hicho kilishaanza kutoa huduma Kwa baadhi ya majengo na baadhi ya majengo bado yanaendelea kukamilishwa hatua Kwa hatua hivyo ukosefu wa umeme umetajwa kuwa ni kikwazo.



Mbali ukosefu wa umeme pia Mwandabila amesikitishwa na kituo hicho kutokamilika kwa wakati muhafaka na ni mojawapo ya vituo vya afya muhimu na kilitengewa fedha kama vituo vingine lakini ujenzi unasua sua.

Mwandabila amesema Kituo cha afya cha Chapwa, Mpande, na Chipaka vimekamilika kwa asilimia 100 na vinafanya kazi lakini hiki cha Mwaka kati bado kimedoda hivyo alitaka majibu ya sababu ya kusua na hata umeme haupo.


Afisa mtendaji kata hiyo Mwashilindi Mwashilindi ametolea ufafanuzi changamoto hiyo akimueleza mbunge kuwa sababu kuu ni umeme unahitajika kwa asilimia kubwa kwani kazi za hapo wakati mwingine wanalazimika kuwasha genereta na kuongeza gharama zisizo na ulazima

"Mh.Mbunge Kuhusu kutokamilika kwa wakati kwa baadhi ya majengo inatokana na ukosefu wa umeme , mafundi wanashindwa kujenga usiku na mchana kutokana na ukosefu wa umeme na wakti mwingine tunawasha Jenereta tunaongeza gharama"alisema .

Kutokana na majibu hayo Mbunge Mwandabila ambaye ni kipenzi kikubwa cha wanachi mkoani humo alilazimika kumpigia simu meneja tanesco mkoa wa Songwe kujua sababu ya eneo hilo kutokuwa na umeme huku akimuagiza kupeleka haraka.


Akipoke maagizo hayo ya Mbunge kwa njia ya simu meneja huyo aliahidi kuipeleka huduma hiyo mwanzoni mwa wiki ijayo

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa