Maafisa Ugani Ileje wakabidhiwa vitendea kazi,wamshukuru Rais Samia
Na Ibrahim Yassin,Songwe
Maafisa Ugani katika Halmashauri ya Wilaya ya Ileje mkoani Songwe wametoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu kwa kuwapatia vitendea kazi ikiwemo Vishikwambi, Gwanda pamoja na Pikipiki.
Akizungumza leo Agosti 28/2024 wakati wa kukabidhi vifaa hivyo Mkuu wa Wilaya ya Ileje Farida Mgomi amewasihi Maafisa hao kuvitendea haki vifaa hivyo ili viweze kuleta tija na mapinduzi ya kilimo wilayani humo.
Amesema pia vitasaidia kuweka msukumo mkubwa katika kuhakikisha wananchi wanazalisha mazao ya kimkakati na kibishara ikiwemo mazao ya Kakao, Pareto, Iliki pamoja na Kahawa.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje Nuru Waziri Kindamba ametoa rai kwa Maafisa hao kuhakikisha wanasimamia na kutoa elimu ya kitaalamu hususan kwa wakulima ngazi ya vijiji katika suala zima la uzalishaji wa mazao.
Kindamba amesema hali ya hewa ya Wilaya hiyo inaruhusu uzalishaji wa mazao ya aina mbalimbali kutokana na kuwa na utofauti wa hali ya hewa kwa kila ukanda ndani ya Wilaya ya Ileje.
Zoezi hilo la kukabidhi vifaa limefanyika mapema leo Agosti 28, 2024 katika Ukumbi wa Halmashauri hiyo huku viongozi mbalimbali wakiudhuria zoezi hilo.
Ifahamike kuwa Rais Dkt Samia kwa kutambua umuhimu wa sekta ya kilimo mwanzoni mwa utawala wake alitoa Bilioni 150 kuwapunguzia makali wakulima .



Comments
Post a Comment