Kipija awapiga tafu Wavuvi kwa kuwajengea vyoo kwenye kambi la uvuvi



Na Ibrahim Yassin,Kyela.

SIKU chache baada ya chombo hiki kuripoti taarifa ya wafanyabiashara na wavuvi Mwalo wa Kafyofyo kijiji cha Njisi kata Kanjumele wilayani Kyela Mbeya kujisaidia vichakani kwa kukosa vyoo hatimaye mdau wa maendeleo Gabriel kipija amekabidhi matundu 4 ya vyoo.

Mwalo huo wenye watu zaidi ya 3,000 wanaofika katika mwalo huo kwa maana ya wavuvi 500 na wanunuzi 2500 wanakumbwa na ukosefu wa vyoo banda la kupumzikia, nyumba yenye majokofu ya kuhifadhia samaki na barabara.

Kutokana na changamoto hiyo inayohatarisha usalama wa watu hao tulifika eneo hilo kuzungumza na watu hao pamoja na viongozi wa serikali kujua kiini cha tatizo na namma ya kulitatua.

Mwalo wa Kafyofyo ni kitega uchumi kikubwa cha mapato ya halmashauri huku vijana wengi wakipata ajira ya uvuvi na wengine wakiacha kukaa vijiweni wakianzisha biashara ya samaki na kujiingizia vipato.
Pia Mwalo huo ni chanzo kikubwa cha mapato ya halmashauri inayodaiwa kuwa na wavuvi na wamiliki wa vyombo vya uvuvi na nyavu 500 wanunuzi wakiwa 2500.

Akizungumza leo na chombo hiki mdau wa maendeleo ambaye pia ni mwenyekiti wa halmashauri mstaafu wilayani humo Gabriel Kipija ame sema alipopata taarifa hizo alishikwa na butwaa.

Alisema katika Mwalo huo mita chache ni eneo lake liitwalo Peponi beach kuna vyoo vya matundu 4 ambapo ameamua kuwakabidhi wavuvi hao ili vitumike wakati halmashauri kujipanga kujenga.

""Mimi Beach yangu iitwayo Peponi ipo jirani na Mwalo huo nami nilikumbwa na uharibufu wa mazingira baada ya maji ya mvua kuharibu eneo langu lakini vyoo vipo safi nimeamua kuwapa wavuvi na wanunuzi wavitumie"alisema Kipija.



Peter Mwantimwa ni mfanyabiashara katika mwalo huo alisema kitendo cha mdau huyo aliyewai kuwa diwani kata ya Serengeti kuwapa vyoo kimewaokoa na janga la kupata homa za milipuko kwa ni kitendo cha kujisaidia vichakani kiliwapa hofu.

Oscar Mwamakula mnunuzi alisema wamelalamikamika miaka mingi kuhusu banda la kujihifadhi pamoja na vyoo kwani vilivyokuwepo viliharibiwa na maji ya mvua na kwamba kwa kuwa wanaendelea kutoa ushuru wajengewe banda kwa kuwa wamepewa vyoo vya peponi.

Mboka Mwankosole mnunuzi alisema wanamshukuru mdau wa maendeleo kwa kuwapa vyoo ila wanaomba wajengewe banda la kujihifadhi kwani msimu huu wa jua hawana sehemu ya kujipumzisha jua na mvua vinawaishia mwilini.

"Mwaka jana halmashauri ilianza ujenzi wa banda lenye uwezo wa kuhifadhi watu 50 kwa Milioni 6 wakati wao wapo 3.000 na kibaya zaidi ujenzi umekwama ukiwa asilimia 10 na fedha hazijulikani zilipo"alisema Mwankosole.

Juma Mwaipopo mwenyekiti wa wamiliki na watumia vyombo vya uvuvi majini alisema upatikanaji wa vyoo hivyo kutawaokoa kupata maradhi kwani badala ya kujisaidia vichakani na kwenye maji sasa watajisitili katika vyoo hivyo.

Alisema baada ya kupewa vyoo hivyo bado ombi lao kuu ni umeme, wajengewe banda la kupumzikia ,banda la majokofu ili samaki wakibaki waweze kuwahifadhi ili wauzwe kesho yake wakifanyiwa hivyo watakuza kipato chao mara dufu.

Said Mwamambi Katibu wa mwalo huo alisema malalamiko ya watu hao sasa yatapungua kwa kuwa wamepata kujisitili kwenye vyoo vya Peponi baada ya kupewa na Mdau Kipija lakini bado wan asisitiza watatuliwe changamoto zilizobaki.

Alisema siku samaki wakikamatwa kwa wingi fedha inayokusanywa kwa ajiri ya ushuru kwa siku inafika hadi laki 5 na kwamba wanaomba sehemu ya ushuru na tozo hizo zirudi forodhani kuondoa changamoto zilizopo katika Mwalo huo.

Tangulini Mwambopo mtoza.ushuru wa halma shauri ,alisema upatikanaji wa vyoo hivyo utarahis ishwa kukusanya ushuru kwani ilikuwa ni ngumu kukusanya kwani baadhi ya watu walikuwa wanagoma kulipa kwa madai ya ukosefu wa vyoo na huduma zingine.


Ally Mlaghila Jumbe Mbunge Jimbo la Kyela alisema ni kweli hali ipo hivyo na sasa Mhe Kipija ametoa vyoo vya peponi Beach nami nitaenda kuzungu mza na wavuvi na wanunuzi kujua namna zaidi ya kutatua changamoto zao.

Katule kingamkono Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya hiyo licha ya kukiri uwepo wa changamoto hizo alisema wapo kwenye mikakati ya kuweka miundombinu rafiki eneo hilo. Ikiwemo kujenga banda la kupumzikia na vyoo vingine vya kisasa

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa