KAMANDA SENGA AKAGUA UJENZI VITUO VIDOGO VYA POLISI NA MAENEO YA UCHIMBAJI SONGWE.




Na Mwandishi wetu,Songwe

Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe  (SACP) Au gustino Senga Jana alifanya ukaguzi na kuvitambua vituo vidogo na vikubwa vya ununuzi wa madini ya dhahabu wilayani Songwe.

Akiwa kijiji cha Paramela na mji wa Mkwajuni makao makuu ya wilaya kamanda Senga alikagua na kuona uwekezaji wa wachimbaji Madini huku akiahidi akiwahakikishia ulinzi wa mali zao na kufanya biashara kwa usalama.


Aidha,Senga alisema jeshi linaendelea kuwa karibu na jamii kwa kutoa elimu na kuwajengea uelewa kuhusu masuala ya uhalifu na ukatili wa kijinsia ili jamii iendelee kuchukia matendo yote maovu.

Alisema anahitaji ushirikiano wa kutosha kati ya wafanyabiashara na wananchi wa kawaida ili kutoa taarifa kwa Jeshi hilo ili kuzuia na kukome sha vitendo hivyo katika jamii.

"Jeshi lipo karibu nanyi hivyo pindi muonapo viashiria vya uharifu ukatili wa kijinsia,mauaji na viashiria vingine vya uharifu toeni taarifa kwa jeshi la polisi ili tushughulike na wahalifu hao " alisema Kamanda Senga.



Katika ziara hiyo kamanda Senga aliambatana na mkuu wa kikosi cha kutuliza Ghasia mkoa SSP Shija Kadogosa na mkuu wa Polisi wilaya ya Songwe SSP Maria Kway  walifanikisha ukaguzi huo.

Kabla ya kwenda wilayani Songwe Kamanda Senga alifanya ukaguzi wa Jengo la ofisi ya Kamanda mkoa wa Songwe linalojengwa eneo la Nselewa wilaya ya Mbozi ambao ujenzi wake bado unaendelea.


Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa