Familia yadhamilia kumuona Rais Ikulu kupigania haki waliyopokwa na kanisa



Na Ibrahim Yassin,Songwe

FAMILIA ya Mwambande Kalinga (50) mkazi wa mtaa wa Mantengo 'B' kata ya Vwawa wilayani Mbozi mkoani Songwe, inajiandaa kwenda Ikulu Chamwino jijini Dodoma kumuona Rais Dkt, Samia kutoa dukuduku lao.

Kalinga amemwambia Mwandishi wa habari hizi jana kuwa ameamua kwenda Ikulu kumuona Rais baada ya kanisa la Moravian usharika wa Vwawa kubomoa nyumba zake 2 na kufyeka mazao kwa madai kuwa eneo hilo ni la kwao.

Mbali na kubomolewa nyumba 2.pia mazao mbalimbali iliwemo miti na kahawa anadai ilifyekwa huku akiachwa akiishi kwa shida na familia yake.



NoAlisema miaka ya nyuma eneo hilo lenye hekali 700 lilikuwa likitumika na muwekezaji ambaye ni Mzungu alipoondoka walikuja wawekezaji wengine na baadae akaja mzee Zebedayo Chungu aliyekaa eneo hilo kama muwekezaji.

Anasema baada ya Mzee Chungu kukaa hapo alimgawia baba yake hekari 12 wakiwemo watu wengine ambao walijenga nyumba za kuishi huku sehemu nyingine wakifanya shughuri za kilimo.

Anasema baada ya baba yake kufariki waliendel ea kulitumia eneo hilo lakini siku za hivi karibuni alishangaa kuona nyumba zinabomolewa na ali pohoji aliambiwa eneo limeuzwa kwa kanisa la Molavian.

Anasema baada ya hapo alienda kushitaki baraza la ardhi Vwawa lakini hakupata msaada na ndipo alipoenda wizara ya ardhi Dodoma ambako nako hakufanikiwa ambapo kwa sasa anajipanga kwenda Ikulu Chamwino kumuona Rais.

"Ndugu mwanahabari eneo hili alipewa marehemu baba yangu na mzee Chungu na kujenga nyumba 2 lakini anashangaa kuona eneo ekali 36 zikiwemo ekali 12 za kwangu zikiuzwa bila kuambiwa wakati wapo katika eneo hilo zaidi ya miaka 10"anasema.

Anasema baada ya kulalamika na kuomba msaada maeneo mbalimbali hajapata msaaada huku familia yake ikilala nje kwa zaidi ya siku 7 hadi alipopewa hifadhi na jirani yake anaamua kwenda kuitafuta haki kwa Mh,Rais Dkt.Samia.

Kwa upande wake mzee Zebedayo Chungu amekiri kuuza eneo hilo akidai kuwa ni mali yake na kwamba eneo alilowapatia familia hiyo hajaligusa kw ani aligawa na ni mali yao eneo lake ndilo alilouza kwa kanisa.

Mwenyekiti wa mtaa wa Mantengo' B' Magreth Kabuje anakiri eneo hilo kuuzwa pamoja na nyumba kubomolewa na kwamba wakati mgogoro huo umeibuka yeye alikuwa bado hajawa kiongozi.

Joyce Kasebwa mwanasheria anayesimamia Kanisa anakiri kuwa eneo hilo ni mali ya kanisa walinunua kwa mzee Chungu na nyumba za mlalamikaji zilibomolewa kwa amri ya mahakama baada ya kushinda kesi akishindwa kulipa fidia ndani ya siku 4.

Frida Mwasulama msajiri wa ardhi mkoani Songwe anasema kanisa limenunua kihalali eneo hilo na kesi ilivyoenda mahakamani kanisa lilipewa ushindi na kukazia hukumu hadi kufikia hatua ya kubomoa nyumba zilizokuwepo.


Anasema mahakama ndiyo yenye haki ya kutoa maamuzi , Mwambande Kalinga katika kesi namba 3 ya mwaka 2018 aliyolishitaki baraza la wadhamini wa kanisa la Moravian ,kanisa lilipewa ushindi.

Anasema baadae Kalinga alikata rufaa katika mahakama ya ardhi Mbeya kesi namba 243/2020 lakini rufaa yake ilikataliwa kwa kuwa ilikuwa nje ya muda na aliomba tena kwa mara nyingine na kukubaliwa katika kesi namba 1/2023.

Anasema baada ya kukubaliwa pande zote 2 ziliitwa kutoa maelezo ambapo baraza la wadhamini wa kanisa la Moravian lilipewa ushindi na kutakiwa kulipwa Tsh, Milioni 4.728.000 kama fidia ambapo ardhi yake Mwambani Kalinga iliuzwa.

Anasema kampuni iliyopewa tenda ya kuuza mali zake ni Fagio Broker ya jijini Mbeya ambayo ilitakiwa kupewa nauli 250.000 na gharama ya kukama ta mali Tsh, 236.000 ambayo imeuza ardhi ya mlalamikaji kufidia fedha hizo.

Hata hivyo Mwandishi Mfukunyuzi wa Dira kamilifu akaenda mbali zaidi na kuzungumza na ofisi ya mkuu wa wilaya wakati huo ambapo afisa tarafa ya Vwawa Haji Khamisi aliyehamishwa Taarafa ya Kamsamba ambaye alieleza hali halisi.

Khamis anasema mzee Chungu ameuza eneo hilo kimakosa kwani hana uhalali, aliishi hapo kama m uwekezaji baada ya muwekezaji mzungu kuondoka na eneo kubaki kuwa mali ya serikali.



Anasema baada ya ofisi ya mkuu wa wilaya kubaini hilo walimwita mzee huyo na kumhoji sababu ya kuuza eneo hilo huku akijua ni mali ya serikali ambapo aliomba radhi na kutakiwa ardhi irudi mikononi mwa serikali.

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa