DED MPENDA AITAKA IDARA YA AFYA KUONGEZA KASI UTOAJI ELIMU KWA JAMII.



Na Ibrahim Yassin,Rukwa.

IDARA ya afya wilayani Kalambo mkoani Rukwa imetakiwa kuongeza kasi ya utoaji wa elimu kwa wananchi umuhimu wa ujenzi wa vyoo bora kuepuka maradhi yakiwemo ya kuambukiza.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Kalambo Mkoani humo Shafii Mpenda wakati alipokutana na timu ya kampeni ya hamasa ya mtu ni afya kutoka wizara ya afya

Mkurugenzi huyo ameitaka idara ya afya wilayani humo kuongeza kasi utoaji elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa ujenzi wa vyoo bora ili kuepukana na milipuko ya magonjwa ikiwemo kipindupindu.

" lengo la serikali ni kuiwezesha jamii kuwa na vyoo bora kutoka asilimia 74 mwaka 2023 na kufikia asilimia 100 ifikapo 2023 na kusisitiza idara ya afya wilayani humo kuhamasisha jamii kuboresha usafi wa mazingira katika makazi, biashara na maeneo ya umma".amesema.

Licha ya hilo amesisitiza jamii kubadili tabia kuhusu ulaji unaofaa na mtindo wa maisha ikiwemo kufanya mazoezi ya mwili kwa njia ya michezo ili kuboresha afya kwa kuwa na utaratibu endelevu wa kufanya mazoezi ya mwili.

Afisa afya mkoani humo Martine Emmanuel amesema jamii inawajibu wa kupambana na kila aina ya unyanyapaa dhidi ya wanawake au wasichana walio katika hedhi ikiwa ni pamoja na kujiepusha na aina za unyanya paa na mila zilizopitwa na wakati.

"Kauli na ushauri wa mkuu wa wilaya inapaswa kufanyiwa kazi,kwani nyumba ni choo hivyo idara yangu itaongeza kasi ya utoaji elimu na ushauri kwa jamii juu ya ujenzi wa vyoo bora"alisema.

Ameongeza kuwa kupitia kampeni hiyo wanahamasisha na kusimamia jamii kuwa na mazingira safi na salama ikiwemo ujenzi wa vyoo bora na utunzaji wa mazingira ili jamii kuwa na afya njema.

Imekuwa ni kawaida ya baadhi ya kaya kwenye baadhi ya wilaya hasa jamii ya wafugaji kutokuwa na utamaduni wa kujenga vyoo bora hivyo kupitia elimu hiyo wataondokana na tabia hiyo.

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa