Chuo cha DIT kupata kituo cha Polisi RPC aongoza kikao kuweka mikakati
Na Ibrahim Yassin.Songwe
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Augustino Senga ameongoza Kikao kwa ajili ya maandalizi ya ujenzi wa Kituo cha Polisi katika Chuo cha D.I.T kilichopo Kijiji na Kata ya Myunga, Wilaya ya Momba.
Kikao hicho kimefanyika jana Agosti 27, 2024 katika Ofisi ya Mkuu wa Chuo Dkt.Lujaji Makamo ambapo kituo hicho cha Polisi kitajengwa katika eneo la chuo kwa ushirikiano kati ya Chuo, Wananchi wa eneo hilo pamoja na Jeshi la Polisi.
Kamanda Senga amesema Lengo la kujenga kituo hicho ni kuimarisha usal ama wa mali za Chuo na Wananchi wa maeneo jirani na kuongeza hali ya usalama wa raia na mali zao.
Aidha, Kamanda Senga ameongeza kuwa lengo la ujenzi huo utaanza mara baada ya taratibu za kura thimisha ardhi utakapokamilika ambao upo kwenye mchakato mzuri.
Sambamba na hilo, Dkt Makamo amelishukuru Jeshi la Polisi kwa kuendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali katika jitihada za kubaini, kuzuia na kutanzua uhalifu na wahalifu ili jamii iendelee kuwa salama.
Wananchi kwa upande wao wakiongozwa na Ester Kileo amesema jeshi la polisi limefanya jambo zuri kujenga kituo eneo hilo kwani wao ni wakulima na wafugaji hivyo mbali na usalama wa chuo hata wananchi watanufaika.



Comments
Post a Comment