CHADEMA Momba yawataka Wananchi kuwakataa viongozi waliopo kwa kutowachagua tena kwani wameshindwa kuwatumikia


Na Mwandishi wetu Momba.

Viongozi wa wa chama cha Demokrasia na.Maendeleo (CHADEMA) kata ya Mpapa bonde la Kamsamba wilayani Momba mkoani Songwe wamewataka wananchi kuacha kuwachagua viongozi waliopo kwa kuwa wameshindwa kuwatumikia.

Akizungumza leo August 7/2024 kwenye mkutano katika kijiji cha Masanyinta katibu wa chadema kata ya Mpapa Edmund Simbeye alisema suala la stakabadhi gharani ni moja ya sababu wakulima kutonufaika na mfumo huo.


Alisema suala la stakabadhi gharani linahitaji elimu zaidi kwa wakulima kuliko ilivyo hapa Momba wanawalazimisha kuuza mazao hasa ufuta stakabadhi gharani ambako kumejaa utata.

"Kuna ubabaishaji uliopo katika mfumo huo unao fanywa na viongozi wa kata na halmashauri kwa ujumla wamewaweka watu wa kununua mazao ukiwemo ufuta kwa bei ya kilanguzi huku wakulima wakiendelea kuwa masikini".alisema.

Nae Dinis Kasonso katibu mwenezi kata ya Kamsamba alisema kilimo ni mkombozi katika kujikwamua kiuchumi lakini kwa wilaya hiyo ni kilio kila kona huku huduma muhimu iliwemo sekta ya kilimo na afya ni majanga matupu.

Alisema uonevu mkubwa kuona mkulima anakopa fedha za riba kulima Ufuta kwa shida na mateso leo akivuna anapewa masharti jinsi ya kuuza hali inayodidimiza uchumi wa mkulima.

"Katika siku tuliyoibiwa ni kipindi hiki wanalazimisha wakulima kupeleka ufuta Godauni la Kamsamba wakidai bei ni 55.000 hadi 60.00 kwa debe la lita 20 alafu anapewa 30.000 hadi 35.000 wakati tayari ufuta umebebwa ukiwa gharani" alisema.

Alisema mkukima anashindwa kulipia ada kwa watoto shuleni huku michango ikiumiza vichwa wananchi na kwamba tunahitaji mkulima auze mazao yake anapotaka ili aweze kulipa ada wakati sahihi na kuboresha maisha yake.


Nae Abdul Ntila mkazi wa Mkonko alisema yeye ana mambo matatu ya kusema moja ni Mbunge Condester Sichalwe amewaweka kuwa ni daraja la kupata mafanikio wakati wakulima wa Momba wanahagaika yeye yupo Dodoma na anajua hilo kwa kuwa ni daraja la kuwakandamiza wananchi yupo kimya.

Alisema lengo la kuchagua mwenyekiti na timu itakayo simamia masuala yote ya wakulima ili kuhepuka kunyonywa na viongozi wapigaji wanao wanyonya wakulima.



"Alisema Rais Dkt, Samia Suluhu anawajali sana wakulima ndiyo maana aliongeza bajeti katika sekta hiyo lakini viongozi wa chini ngazi ya wilaya wanaumiza wakulima" alisema.

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa