Watu wawili mkoani Songwe wauawa kikatili huku Polisi wakihaha kuwasaka wahalifu




Na Ibrahim Yassin, Songwe

JESHI la.polisi mkoani Songwe linafanya oparesheni kuwasaka watu walioendeha mauaji ya watu wasio na hatia huku likitangaza kiama kwa wata kaokamatwa kuhusika na mtukio hayo.

Hatua ya msako huo imekuja baada ya watu wasiojulikana wamemuua mzee Kamunya Nsambo (58) mkazi wa kijiji cha Nambizo wilayani Mbozi mkoani Songwe huku akitupwa katika msitu wa Mkukwe katika kijiji cha Isenzanya mwili wake ukiwa umeharibika.

Akizungumza leo Julai jana kaimu kamanda wa.polisi mkoani humo ASP_ Gallus Hyera amesema mtu huyo alitoweka nyumbani kwake siku kadhaa na alikutwa kwenye msitu huo baada ya mbwa kuonekana wakiwa na vipande vya nyama za marehemu huyo ambaye mwili wake uliharibika.

Amesema baada ya kuukuta mwili huo ambapo mtu huyo alitoweka Julai 11 mwaka huu na mwili kukutwa ukiwa umeharibika na baadhi ya sehemu za mwili wake kuliwa na wanyama wakali waliamuru azikwe kwenye msitu huo.

Amesema kulikuwepo na upotoshwaji na baadhi ya vyombo vya habari vilivyoeleza kuwa ".watu wasio fahamika wamemuua mzee Kuminya Nsam bo kisha kunyofoa mguu na mkono kitu ambacho sio kweli"amesema kamanda Hyera.

Katika hatua nyingine amesema wakiwa katika operesheni walifanikiwa kumkamata Masunga Kisabo (47) mkazi wa Iyanga _Njelenje Mbeya vijiini akituhumiwa kufanya mauaji siku ya Julai 16 /2024 katika kitongoji cha Namarangu kijiji cha Itindi kata ya Galula wilayani Songwe.

Amesema jeshi hilo lilimkamata kijana huyo baada ya kugundua kumuua Monica Mahengule (65) akiwa chumbani kwake ambapo alikatwa na kitu chenye ncha kali kichwani na kupelekea kifo baada ya kuvuja damu nyingi

Amesema baada ya kumhoji mtuhumiwa alikili kuhusika na mauaji ya Monica na kusema kuwa alikodiwa kutekeleza maujai hayo akishirikiana na watu wengine ambao jeshi la polisi linaendelea kuwasaka.

Aidha kaima.kamanda huyo amesema jeshi la polisi linatoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Songwe kutojichukulia sheria mkononi na linawataka watoe taarifa pindi waonapo viashiria vya uarifu na matukio ya ukatili ili waweze kuyafanyia kazi.

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa