Wananchi watakiwa kutumia nyumba za ibada kutenda mema
Waamini wa kanisa la T.A.G Calvary Christian Center lililopo Majengo Mjini Tunduma kwa Mchungaji Eliud Amos Kalinga wametakiwa kuendelea kufanya matendo mema na kukemea matendo maovu jambo ambalo litasaidia kupunguza vitendo viovu kwenye jamii....anaripoti Ibrahim Yassin.Songwe
Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Augustino Senga, Julai 07, 2024 wakati akitoa elimu ya Polisi Jamii katika kanisa hilo lililopo wilaya ya Momba Mkoa wa Songwe.
Kamanda Senga alisema "Tumshike Mungu watu ndugu ikiwa ni pamija na kuinjilisha kwenye jamii bila kusahau kuyatenda yale yote aliyoyaelekeza katika biblia takatifu pia kuyaishi ili kutokomeza vitendo viovu katika jamii zetu .
"kwa umoja wetu tusijihusishe na vitendo vya uhalifu na ukatili ikiwa ni pamoja na unyanyasaji kwa watoto" alisema Kamanda Senga.
Kamanda Senga aliendelea kuwasihi waumini wa kanisa hilo waliohudhuria katika ibada hiyo kuac ha matumizi ya ulevi uliopindukia na kutoamini imani za kishirikina ambapo kufanya hivyo kutap unguza vitendo vya ukatili wa kijinsia na unyanya saji dhidi ya watoto.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Polisi Wilaya ya Momba Mrakibu wa Polisi SP Bhoke Simango aliwataka waumini hao kuendea kutoa elimu iliyo tolewa na Kamanda Senga na kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi na hasa katika kuk omesha vitendo vya kihalifu kwenye maeneo yao.
Eliud Kalinga mchungaji wa kanisa hilo, amesema elimu huyo kutokana na umuhimu wake kila ataka pokuwa madhabahuni atakuwa akitoa elimu hiyo ili jamii iishi maisha mema yakumpendeza mungu



Comments
Post a Comment