Wananchi wachanga fedha kujenga kituo cha Polisi
Na Ibrahim Yassin.Songwe
Katika kujihakikishia hali ya usalama wao na mali zao unakuwa salama wakazi wa vijiji vilivyopo kata ya Mbangala wilayani Songwe mkoani hapa wameamua kuchangishana fedha kujenga kituo cha polisi .
Wakizungunza jsna wakazi wa kata hiyo wamese ma Mbangala ni kata ulinayokuwa kwa kasi kuto kana na uwepo wa shughuri za uch imbaji wa dhahabu.kilimo na uvuvi wa samaki hivyo kuna umuhimu wa kituo cha polisi kujebg wa.
Samwel Juma muuza samaki ziwa Rukwa amese ma alipoambiwa kuna mchango wa ujenzi hakusi ta kuchanga kwani wamekuwa wakisafiri na fedh a kwa hofu ya kuvamiwa na wezi hivyo kituo hicho cha polisi kitasaidia kuwa na uhakika wa usalama zaidi.
Nae Suma Kimenya mkazi wa Mbangala ame sema yeye ni mjasiliamali wa kununua dhahabu ukosefu wa kituo cha afya kuliwapa changamoto ya kuficha fedha kwenye nguo za ndani wakihofu kuvamiwa wameamua kujenga kituo cha polisi kujihakikishia uaalama.
Diwani wa kata hiyo Abraham Sambila amesema amefurahishwa na wananchi kuchanga Tsh.29 .766.640 zilizotumika kwenye ujenzi hadi sasa na ana uhakika ujenzi wa kituo hicho utak amilika ma pema huku akisema wafanyabiashara na wawek ezaji watazidi kuongezeka.
Sambila ambaye pia ni mwenyekiti wa halmash auri hiyo ameongeza kuwa kata hiyo inawaweke zaji wengi waliojenga viwanda vya kuchimba na kuchakata madini ya dhahabu hivyo kituo hicho kitawahakikishia usalama kwani polosi watakuw epo muda wote.
Mbunge wa jimbo hilo Philipo Mulugo amesema ujenzi wa kituo hicho ni mwanzo wa ujenzi wa vituo vingine kwenye kata zenye wawekezaji wengi ili kuhakikisha usalama zaidi huku akiwap ongeza wana Mbangala kwa hatua hiyo kwani kata hiyo ni lango kuu la kusafirushia smaki kwenda mikoani.
Akizungumza kwa njia ya simu jana baada ya kuzindua jengo hilo.kamanda wa polisi mkoani Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Augustino Senga amesema amerid hishwa na viwango vya jengo hilo.
Amesema Mradi wa Ujenzi wa kituo cha kata ya Mbangala kilichopo wilaya ya Songwe ambacho kimejengwa kwa nguvu ya wananchi wa kata hiyo na ujenzi wake unaendelea vuzuri japo bado unaendelea.
Baada ya ukaguzi huo alizungumza na maofisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali ambapo aliwataka kuendelea kutekeleza majukumu yao ya kazi za Polisi kwa kutoa huduma bora kwa wana nchi wanaowahudumia ikiwa ni pamoja na kutek eleza maelekezo ya Tume ya haki jinai.



Comments
Post a Comment