Wakazi wa Kyela sasa kunufaika na kiwanda cha kuchakata mafuta ya kula



Na Ibrahim Yassn Mbeya

WAKULIMA zaidi ya elfu kumi wa zao la mawese wilayani Kyela mkoani Mbeya watanufaika na kuk uza thamani ya zao hilo kutokana na kujengwa kwa kiwanda cha kuchakata mafuta ya kupikia na sabuni..

Kiwanda hicho cha Covenant Edible Kyela Cooking Oil kilichoanzishwa na muwekezaji mzawa kinatarajiwa kuanza uzalishaji wiki ijayo huku kikitajwa kuwanufaisha wakulima wa zao hilo.

Akizungumza na mwandishi wa habari mkurugenzi wa kiwanda hicho Babylon Mwakyambile amesema baada ya kumaliza masomo chuo kikuu aliamua kuanzisha kiwanda nyumbani ili kuchakata mafuta na sabuni na kutoa ajira kwa vijana.

Amesema kiwanda hicho kitafanya kazi ya kukamua mafuta ya mbegu ya alizeti (Best Harvest) na Mbegu za mawese ( Kyela Cooking Oil) na kw amba mwezi Julai 22/2024 uzalishaji utaanza rasmi.

Amesema kuwa kiwanda hicho kitakuwa ni mkombozi kwa wakulima ambao wameanza kuunda vikundi vyenye watu zaidi ya elfu 10 watakaoingia makubaliano ya kuuza mawese kwa bei elekezi huku vijana zaidi ya 100 wakitarajia kupata ajira.

""Tunatarajia mwenge wa uhuru utuzindulie kiwanda hiki, lakini kwa muda huu tumeanza kununua mafuta kwa ajili ya kuanza uzalishaji sambamba na kutoa elimu kwenye vikundi vilivyo anzishwa "amesema.

Lutufyo Mwambola mkulima wa zao la mawese amesema ujio wa kiwanda hicho kitaongeza thamani ya mkulima kwani wanalazimika kuuza kwa bei ya chini kutokana na ukosefu wa soko.

Meckson Mwaikambo mkulima amesema wana Kyela walikuwa wakiuza mawese yaliyosafirishwa kwenda Dar es salaam kuchakatwa kuwa mafuta ya kupikia alafu wanayaleta kutuuzia, kwa sasa yatachakatwa hapa hapa na yatauzwa kwa bei ya chini ndani na nje.

Lusekelo Mwaibambe mnunuzi wa mawese (mc huuzi)amesema tangu kiwanda hicho kianzishwe mafuta yamepanda bei awali walikuwa wakinunua Tsh, 30.000 dumu la lita 20.bei ya sasa inayonunuliwa kiwandani hapo ni Tsh,.43.000.

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa