Umoja wa Wazee wajizatiti kukabiliana na mmomonyoko wa maadili na kusimamia haki za Wazee Nchini
Mwenyekiti wa umoja wa Wazee taifa Anyimike Mwasakilali amewataka Wazee kupitia umoja wao kitaifa kulisimamia suala la Maadili Kwa Watoto wao Ili kuwa na taifa linaloheshimika duniani Kwa kuwa na Watu waliostaarabika.
Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake Leo amesema kuwa jamii sasa imepoteza mwelekeo hasa baada ya mmomonyoko wa Maadili hasa Kwa vijana na kuwa Watu wenye uwezo wa kuirudisha jamii katika misingi yake ni Wazee.
Amesema umoja wa Wazee kitaifa umesajiliwa kama taasisi ya kushughulikia masuala yanayowagusa Wazee Nchini lakini pia wanalo jukumu kubwa la kuhakikisha kuwa mambo katika taifa hili yanakwenda vizuri ikiwa ni pamoja na kukemea pale inayoonekana Kuna jambo linakwenda kinyume na ustawi wa taifa .
Mwasakilali amefafanua kuwa Wazee hapa Nchini wanakabiliwa na changamoto nyingi na kuwa kutokana na Hilo wameamua kuanzisha taasisi hiyo ya Wazee itakayowaunganisha Wazee na kuwa na nguvu ya pamoja kupigania Haki zao ikiwa ni pamoja na masuala ya kijamii.
Alidai kuwa toka taasisi hiyo Toka isajiliwe na kuanza kufanya kazi Nchini Oktoba 23,2023 na makao makuu yake yakiwa wilayani Rungwe wamefanikiwa kuwaunganisha Wazee Nchi nzima lakini pia wameweza kuyashughulikia baadhi ya mambo kama Vile soko la Parachichi Rungwe ikiwa ni pamoja na kushirikiana na viongozi wa serikali katika kusukuma ajenda mbalimbali zenye maslahi Kwa taifa .
Baadhi ya Wazee kutoka katika Mikoa ya Rukwa,Ruvuma,Kigoma na Iringa wameeleza Namna ambavyo wameweza kuunganishwa na umoja huo wa Wazee na kuwataka wawe pamoja unyonge wao umetoweka Kwa maana wamekua na nguvu ya pamoja katika kushughulikia masuala yanayowagusa kama Wazee ikiwa ni pamoja na yale ya kijamii na kuwa sasa Wazee wanaheshimika Kwa namna ambavyo wanashughulika na mambo ya kijamii.
Julius Kitao mkazi wa Kijiji Cha Muze Mkoani Rukwa amedai kuwa Kuna mambo mengi walikua wakishindwa kuyakabili kama Wazee lakini umoja huo umewapa nguvu na kumshukuru Mwasakilali Kwa namna ambavyo amekuwa akiwapa nguvu na kuwatia moyo na kuwapa miongozo inayowawezesha kuyafikia malengo Yao.
Anganile Sanga mmoja wa Wazee kutoka wilayani Makete Mkoani NJombe amedai kuwa umoja huo umefanikiwa kuwakutanisha Wataalamu wa kada mbalimbali ambao ni wastaafu na kuwa imewasaidia sana kushughulika na changamoto wanazozipitia na kupata suluhisho ya changamoto zao..
Umoja wa Wazee ni taasisi iliyoundwa kama taasisi isiyokuwa ya kiserikali licha ya kuwa Bado haijafika mikoa yote Nchini mkakati wao mkubwa Kwa sasa ni kulifikia mikoa yote Nchini

Comments
Post a Comment