Mwamengo ajitolea kutengeneza barabara


Na Ibrahim Yassin,Mbeya

Wananchi wa Tarafa ya Unyakyusa (Kyela mjini) na Ntebela ( Kyela Vijijini) wilayani Kyela mkoani Mbeya wamempongeza Baraka Mwamengo kwa kutumia Milioni 7,7 kujitolea kujenga barabara ya kiwango cha vumbi.

Mwamengo kupitia kampuni yake ya Basai General Supplies Ltd, amelima barabara katika kat a mbili za Mbungani na Itunge zenye jumla ya Km 2.2 ambazo gharama yake ni Tsh Milioni saba na laki saba (7,700,000).kuwaondolea wananchi changamoto hasa nyakati za mvua.

Wakizungumza jana gazeti hili, wananchi hao wamesema wilaya ya Kyela ina wasomi wengi wenye nyadhifa mbalimbali serikalini na kwenye taasisi mbalimbali lakini ni wagumu kuchangia maendeleo nyumbani kwao hivyo Mwamengo amefungua mirango.



Abubakari Timba mkazi wa Unyakyusa amesema kitendo cha Mwamengo kutoa fedha zake kuten geneza barabara kimewashangaza wengi kwani Kyela yenye wasomi wengi waliopo kwenye nyadh ifa mbalimbali wamekuwa wagumu kujitolea.

''Ndugu mwandishi barabara hii ipo katikati ya mji ndani ya mamlaka ya mji lakini imekuwa ikifumuka .mashimo ni mengi hali inayotupa shida kusafirisha thamani za ujenzi ikiwemo tofari na mchanga kufunguliwa kwa njia hii kutarahisisha usafirishaji wa bidhaa na kuuweka mji kwenye mandari nzuri''amesema Timba.

Darken Mwakalambo mkazi wa Ntebela ames ema Mwamengo ni mfano wa kuigwa kujenga kilometa 2.2 ni jambo kubwa ameamua kujitole kwa kujenga kyela mjini ambapo siku za hivi karibuni alitengeneza Kyela vijijini.

Afisa miradi wa kampuni hiyo Anthon Mwamkon da amesema hatua hiyo ya kampuni kutengeneza barabara imekuja baada ya ya wananchi hivyo mkurugenzi Mwa mengo anatimiza ahadi kwani viongozi wa serikali na chama cha mapinduzi wa kata mbalimbali walitoa maombi hayo.

""Kuna maombi mengine kwenye kata zilizopo kwenye Tarawa za Unyakyusa na Ntebela zipo mbioni kuteengenezwa hivyo kampuni itatimiza maombi hayo siku za hivi karibuni tumeanza na kilometa 2.2 kwa Mil.7.7 tunaendelea kungine "amesema Mwamkonda.



Mkurugenzi mwamengo licha ya kujitolea kut engeneza barabara hiyo pia amekuwa na kawa ida kusaidia shughuri za ujenzi wa miradi ya Afya. elimu. miundombinu na kwenye taasisi za dini ikiwemo kusaidia watoto yatima na watu wenye uhitaji maalum.

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa