Hatarini kupata magonjwa ya kuambukiza baada ya Wavuvi kujisaidia porini kwa kukosekana kwa vyoo
Na Ibrahim Yassn Kyela.
WAVUVI na wafanyanbiashara ziwa Nyasa mwalo wa.Kafyofyo uliopo kijiji cha Njisi kata ya Kajunjumele wilaya ni mkoani Mbeya wapo hatarini kuku mbwa na magonjwa ya mlipuko kwa kujisaidia vichakani, mchangani na kwenye maji kwa kukosa vyoo.
Wakizungumza jana na Gazeri hili wafanyabiashara na wavuvi hao walisema licha ya kulipa ushu ru na tozo mbalimbali za halmashauri lakimi haku na huduma wanazopatiwa huku wakiwa katika mazingira hatarishi.
Peter Mwantimwa mfanyabiashara katika mwalo huo,alisema licha ya choo kilichokuwepo mwaka jana cha matundu 6 kujengwa na mdau Elius Mwakalinga kusombwa na maji hadi sasa hawana pahala pa kujisitiri zaidi ya kwenda vichakani.
Mayasa Kimaro mnunuzi wa.samaki alisema ukosefu wa vyoo imepelekea.wajisaidie kwenye matete na hata kuchimba mchanga waakijisaidia wanafukia havyo mazingira ya mwalo huo ni hatarishi kwa afya zao.
Oscar Mwamakula mvuvi alisema wapo kwenye wakati mgumu kwani kutendo cha kujisaidia kwen ye vichaka wakati wanatoa ushuru halikubaliki kw ani hata kama ng"ombe unamkamua maziwa inap aswa umlishe ili aendelee kukupa maziwa mengi.
Said Mwamambi Katibu wa mwalo huo alisema ni kweli hali hiyo ipo na imatokana na choo kilichopo kusombwa na.maji kufuatia mvua kubwa za mafu riko.
Tangulini Mwambopo mtoza.ushuru wa halma shauri katika Mwalo huo,alisema hakuna maende leo yaliyopo na inatupa wakati myumu kukusanya ushuru watu wengi wanagoma hivyo ni bora wangejengewe
Benald Razaro mvuvi amesema wanalazimika kujisaidia kwenye maji pindi waendapo kuvua na wakiwa nchi kavu wanenda vichakani kisa ukose fu wa vyoo hivyo aliomba halmashauri iharakishe ujenzi kulinda usalama.wa.afya zao.
Juma.Mwaipopo Mwenyekiti wa watumiaji wa vyombo majini aliswma wapo zaidi ya 3.000 wav uvi 500 na wanunuzi 2,000 kila nyavu inalipiwa kila mvuvi analipa na kila ngalawa inatozwa na kila ndoo ya mnunuzi inatizwa ushuru lakini ha wajui fedha zinakokwenda.
Ally Mlaghila Mbunge Jimbo la Kyela alisema ni kweli hali ipo hivyo na imetokana na maji ya mvua za masika kukisomba choo hicho na kwamba atazungumza na mkurugenzi wa halmashauri kuona namna ya kukijenga.
"Ndugu wanahabari maji ya ziwa yaliongezeka yakasomba choo na kuharibu.miundombinu hivyo tutashirikisha wataalam kuona namna ya kujenga choo japo maji bado hayajapungua."" alisema Mlagila.
Katule kingamkono Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kyela licha ya kukiri uwepo wa chang amoto hiyo alisema wapo kwenye mikakati ya ku jenga vyoo vingine hivyo aliwataka wavuvi na wafanyabiashara hao kuwa wavumilivu.



Comments
Post a Comment