Vifo vya kujinyonga vyawashitua Polisi mkoani Songwe
JESHI la polisi mkoani Songwe,limefadhaika na vitendo vya watu kujiua kwa wivu wa mapenzi,ugumu wa maisha na wengine kujiua baada ya kuugua kwa muda mrefu huku likitoa elimu kwa jamii ili waweze kutumia ushauri wa watu wao wa karibu wanaowaamini ili kuhepuka kujiua.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo Januari 29/2/2024 kamanda wa polisi mkoani Songwe Theopista Mall ya,alisema jeshi hilo limeendelea kuimarisha ulinzi na usalama kwa kushirikisha jamii katika kubaini,kuzuia au kutanzua uhalifu kwa kufanya doria,msako na operesheni.
Aidha amesema katika msako huo wameweza kuripotiwa matukio ya wananchi kujiua kwa sababu mbalimbali hali iliyopelekea azidishe kasi ya utoaji elimu kwa jamii ili kuhepuka kujiingiza kwenye matukio hayo ya kujiua.
Amesema siku ya februari 06/2024 majira ya saa 9 kamili katika kijiji cha Igale kata ya Iyula wilayani Mbozi Adam Motela (58) alikutwa amefariki dunia chumbani kwake baada ya kunywa sumu huku mwili wake ukiwa umelala kifudifudi baada ya kunywa pombe kupindukia baada ya kufiwa na mama yake mzazi.
Amesema mama mzazi wa marehemu huyo alifariki Januari 14/2024 na kupelekea kuwa na msongo wa mawazo yaliyopelekea anywe pombe kupitiliza na kusababisha umauti wake na katika chumba chake zilikutwa chupa za bia aina ya Bingwa.
Aidha kamanda huyo alisema mbinu nyingine aliyoitumia ni kunywa sumu ya kuulia magugu aina ya Gramoxsone na nimja pamoja ali zokunywa kwa kuchanganya na bia ainaya Bingwa na kupelekea umauti wake.
Aidha kamanda Mallya aliongeza kuwa siku ya Februari 10/2024 majira ya saa 5 kamili asubuhi katika mtaa wa Nyerere kata ya Chipaka halmashauri ya mji Tunduma,Dotto Mwajombe (20) ali yekuwa akifanya kazi ya kuchenji Fedha za Zambia (kwacha) na shilingi za Tanzania alikutwa alifariki dunia kwa kujinyonga..
Amesema marehemu alikuwa akiishi nyumbani kwa kaka yake nyumba ya uani na kwamba kiini cha kujiua kwa kujinyonga bado haki jafahamika na wao wanaendelea na uchunguzi.
Pia Kamanda Mallya alisema siku ya Januari 13/2024,saa sita usiku katika hospitali ya wilaya ya Mbozi Dicto Shitindi (35) mkazi wa kijiji cha Bara alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu baada ya kunywa dawa ya kuulia magugu aina ya Gramoxone ambapo alijifungua chumbani na sababu bado haijafahamika.
Aliongeza kuwa siku nyingine ya Februari 21/2024 saa kumi jioni katika kitongoji na kijiji cha Ikinga tarafa ya Bundali wilayani Ileje Victor Chamba (24) alikutwa amefariki dunia chumbani kwake kwa kujinyonga na kipande cha shuka,na kwamba uchunguzi ulibaini alikuwa anaugua ugonjwa wa akili.
Aliongeza kuwa mnamo Februari 22/2024 saa nne asubuhi,Kenan Mbiye (50) mkazi wa mtaa wa Kisangani kata ya Muungani halm ashauri ya Tunduma,alikutwa amefariki dunia chumbani kwake kwa kujinyonga akitumia kipande cha waya ya umeme sababu ya msongo wa mawazo.
Amesema marehemu baada ya kuachana na mke wake alikuwa akiishi peke yake akiwa na msongo wa mawazo hali iliyomlazimu ajiue kwa kujinyonga na waya ya umeme akijitundika juu ya mbao za kenchi.
Pia Kamanda Mallya alisema siku ya Februari 26/2020 saa moja kamili asubuhi, Egnasho Simchimba (18) mkazi wa kijiji cha Igamba wilayani Mbozi,ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha nne sekondari ya Shiwinga alikutwa amefariki chumbani kwake baada ya kunywa sumu aina ya Acteric.
Aidha ameongeza kuwa siku ya Februari 23/2024 saa mbili usiku Ibrahim Mbukula (30) mkazi wa mtaa wa Kiwanda kata ya Mlowo wilayani Mbozi alikutwa amefariki dunia baada ya kunywa sumu baada ya mgogoro kindoa wa muda mrefu baina yake na mke wake.
Amesema awali iliripotiwa kuwa taarifa ya kupotea kwake Februari 14/2024 na kukutwa akiwa hali mbaya kwenye msitu wa Mwankonde Februari 15/2024 majira ya saa 11 alfajiri na kukimbizwa hospitali ya Mbozi na alifariki dunia wakati alifanyiwa matibabu na ilibainika alichanganya sumu na soda na kuinywa.
Kamanda Mallya amesema jeshi la polisi linatoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Songwe kuacha kujichukulia sheria mkononi kwa kufanya vitendo vyovyote vya kiharifu na kuwasihi viongozi wa dini na kimila kuendelea kutoa elimu kwa jamii kutumia nyumba za ibada na mikutano ya hadhara.
Amesema utoaji wa elimu hiyo utasaidia kutokomeza janga hilo la watu kujiua ikiwa ni pamoja na kuwataka wananchi pindi wanapopata changamoto za kimaisha waweze kuwashirikisha watu wanao wa amini ili kuweza kuwasaidia kutatua changamoto zinazo wakumba.


Comments
Post a Comment