Milioni 780 kuokoa watu kuuwawa na Mamba mto Ugalla





Na George Mwigulu, Nsimbo.

Serikali inatekeleza ujenzi wa mradi wa maji safi na salama wenye thamani ya fedha ya Mil 780 katika Kijiji cha Katambike kata ya Ugalla Halmashauri ya Nsimbo Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi.

Ujenzi wa mradi huo umeanza kutekelezwa mwenzi April mwaka huu na unatarajia kukamilika mapema mwenzi Novemba na utaokoa maisha ya watu wengi ambao vifo vyao vimeripotiwa kwa nyakati tofauti kwa sababu ya kuliwa na Mamba wakati wakichota maji katika hifadhi ya taifa ya mto Ugalla.

Anna Lupembe,Mbunge wa Jimbo la Nsimbo Mkoa wa Katavi amesema hayo leo Septemba,17,2023  katika kitongoji cha Uvuvini Kijiji cha Katambike Kata ya Ugalla.

Mbunge huyo amesema  kuwa kwa hatua ya ujenzi wa mradi huo upo kwenye  ujenzi wa tanki la maji lenye ukubwa wa lita Mil  za ujazo sambamba na uwekaji wa mabomba kwenye maeneo mbalimbali ya kata ya Ugalla unaendelea.

´Ninafahamu na ndio maana nikaelekeza na kuomba fedha serikali ili kuhakikisha tunapata tenki kubwa la maji hapa katika kijiji cha Katambike na kwa sasa ninyi wenyewe mnamuona mkandarasi yupo anaendelea na kazi´´ Amesema Lupembe.

Aidha ametoa ahadi  kwa wananchi wa kitongoji caha Uvuvini atawachimbia visima vya maji ili kuwa sehemu ya kuimaruisha zaidi huduma ya maji.





Lupembe amesema suala la watu kuliwa na mamba kwa sababu ya ukosefu wa maji safi na salama ni jambo ambalo akiwa mbunge kwa muda mrefu limemnyima usingizi na kama mwanamke hapendezwi kuona wanawake wengine wakiteseka.


Aidha amesema licha ya hatua kubwa inayofanyika ya kuimarisha miundombinu ya maji lakini pia amewasiliana na uongozi wa TAWA kuhakikisha mamba wanavunywa katika hifadhi ya taifa yam to Ugalla.


Naye Mwenyekiti wa halmashauri ya Nsimbo,Halawa Charles Malendeja amesema kuwa serikali imejipanga kwa dhati kuhakikisha inamtua ndoo mwanamke ambaye kwa muda mrefu amekuwa muhanga wa kuteseka kuchota  maji.



Amebainisha kuwa jukumu ambalo wananchi kwa sasa wanapaswa kufanya ni kulinda miundombinu inayowekwa ya maji katika kata ya Ugalla ili kuhakikisha kila mwananchi anafikiwa na huduma ya maji.


Kwa upande wa baadhi ya wananchi wa kata ya Ugalla,Mariamu Hassain amempongeza mbunge kwa kazi nzuri ya kuendelea kuhakikisha wananchi wake hawapati matatizo yanayorudisha nyuma maendeleo yao,



Comments


Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa