MBUNGE MULUGO AKABIDHI PIKIPIKI KWA WATENDAJI WA KATA TATU, ASEMA ZITASAIDIA KURAHISISHA UKUSANYAJI MAPATO.


Na Ibrahim Yassin,Songwe 

Mbunge wa Jimbo la Songwe, Mhe. Philipo Mulugo (Papaa) amekabidhi pikipiki kwa watendaji wa kata tatu za Halmashauri ya Wilaya ya Songwe ili ziweze kuwasaidia watendaji hao kurahisisha kutimiza majukumu yao.

Amesema moja ya kitendea kazi muhimu katika ukusanyaji mapato ya halmashauri ni pikipiki ambazo zitamrahisishia kufika maeneo mbalimbali kwa wakati kukusanya mapato.

Amesema wilaya ya Songwe ni moja ya wilaya yenye masoko mengi ya minada hivyo pikipiki hizi zitafanikisha mtendaji kufika kwa wakati na kutimiza majukumu yake.

Mbunge Mulugo amekabidhi pikipiki hizo leo Jumanne Agosti 27, 2024 kwa watendaji wa Kata za Mwambani, Kanga na Udinde ambazo ni kata ziliz okuwa zimebaki kukamilisha kata zote 18 kupata pikipiki.

Naye mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wlaya hiyo  Secilia Kavishe amesema anaipongeza serikali ya awamu ya sita kuona umuhimu wa kutoa pikipiki kwenye kata zote 18 hali itakayorahisisha shughuri za kiutendaji kwa maafisa hao.


Akimuwakilisha mkuu wa wilaya hiyo, katibu tawala Godfrey Kawacha  amesema upatikanaji wa pikipiki hizo anaamini kasi na weledi katika uwajibikaji utaongezeka huku akiwataka watendaji hao kutozitumia kubeba mizigo.

Mwenyekiti wa halmashauri ya Songwe Abraham Sambila mbali na kuipongeza serikali kwa pikipiki hizo pia amewataka watendaji hao kutozitumia kubebea abiria na badala hake waongeze jitihada za uwajibikaji.

Comments